Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

SASA UNAWEZA KUPATA KITABU CHA SIMULIZI YA MZEE MADIBA TOKA ANAZALIWA MPAKA KUFARIKI KWAKE KWA TSH. 3500/=

$
0
0

Ndugu zangu,


Juzi Jumapili tumemzika Mzee Wetu Madiba. Na leo hii nimekamilisha kazi ya kukusanya simulizi zake na kuzifanya kuwa kijitabu kidogo cha kurasa 80. Ni simulizi inayotokana, kwa kiasi kikubwa na maandiko yake Nelson Mandela mwenyewe, kwenye kitabu chake; " Long Walk To Freedom, 1994)

Nimeifanya kazi hii kutokana na maombi ya wasomaji na wafuatiliaji wengi wa kazi zangu. Nami nimejisikia nina jukumu la kutumia elimu, maarifa na kipaji changu katika kuifanya kazi hii ya kijamii.


ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Ni imani yangu kuna watakaofaidika na yaliyomo kwenye kijitabu hiki. Kuna ambao wamesahau tu, wanahitaji kukumbushwa, lakini, kuna ambao, watakayoyasoma yatakuwa ni mapya kwao. Ni maarifa mapya. Na wahenga walisema; hakuna ziada mbovu.

Tangu utotoni nimependa sana kusoma vitabu. Na nimetamani kuwashauri watu wengi zaidi wasome vitabu. Naamini, kuwa dunia yote imo ndani ya vitabu. Na hata kama huna uwezo wa kifedha kusafiri, basi, kupitia vitabu, unaweza kusafiri kifikra, na utaona yote unayotaka kuyaona. Na utawajua hata wale ambao hujapata kukutana nao.

Naam, kupitia kazi hii, ni imani yangu nitawahamasisha wengine kupenda kusoma vitabu.

Maggid Mjengwa.
Iringa.
0754 678 252

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>