Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

HAYA NI MAMBO SITA(6) YANAYOWEZA KUKUZA AU KUUA UBUNIFU WAKO

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Ulimwengu tulionao na vitu vinavyoendelea vipo kwa sababu kuna watu waliweza kutumia muda wao na wanaendelea kutumia muda wao kubuni vitu mbalimbali kila siku. Hivyo basi kuna watu ambao wanajaribu kuja na wazo au kitu kipya kila siku huke wengine wakijiuliza na kusema hawawezi kubuni kitu kipya kabisa. Tofauti kati yetu na watu wengine ambao ni wabunifu ni namna ambavyo tunayachukulia mambo. Huwa tunaamua kushindwa kabla ya kuanza hata kufikiri, jifunze siri chache hapa;

1. Usikae muda mrefu bila kupumzika. Hapa tunazungumzia uwezo wako wa kufikiri na kufanya mambo unapungua pale unapokuwa umechoka au kutokupata muda mzuri wa kulala. Unahitaji kupata usingizi wa kutosha ili uweze kuendelea kutafakari na kufanya vizuri siku inayofuata.

2. Usisubiri watu wengine wakuonyeshe na kukuelekeza kitu cha kufanya. Kila wakati jifunze na jaribu vitu vipya, jipe changamoto ya kitu usichokijua na ujifunze uone mwisho wake utakuwaje. Vile vile uliza au omba msaada sehemu ambayo unaona inakusumbua kwa kiasi fulani au kuzuia wewe kuweza kuendelea mbele.

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI



3. Usifanye kitu peke yako au usipende kufanya vitu kwa uchoyo wa mawazo. Hakuna mtu duniani alifanikiwa peke yake, kila unayemuona amefanikiwa ana kundi la watu nyuma yake ambalo anafanya kazi nalo. Hao ni watu ambao anashirikisha mawazo yake huko, wanampa changamoto na kurekebisha au kusahihisha pale ambapo hapajakaa vizuri na kuendelea mbele. Unapoamua kufanya kila kitu mwenyewe inafika mahali huwezo kwenda mbele tena, kwakuwa kila mtu ana kikomo cha mawazo na utendaji.

4. Usipende kuiga mambo kwa watu wengine. haimaanishi kama fulani anafanya kitu fulani kinafanikiwa basi na kwako kitafanikiwa hivyo hivyo, hayo ni mawazo finyu kabisa. Kwa namna moja ama nyingine yanaendelea kututesa sana hapa tanzania , hasa kwenye mfumo wetu wa biashara ndio maana unaweza ukakuta vilabu vya pombe vinne sehemu moja ila wamiliki tofauti. Baada ya muda fulani nyingine zinakufa na hawajui kwanini biashara yao imekufa, kumbe waliiga tu hawakufanya upembuzi yakinifu kuhusu biashara hiyo.

5. Usiwe mwepesi wa kuhukumu jambo na mbishi. Kitu chochote kinapotokea inakubidi uchukue muda na ufikirie kabla ya kutolea maamuzi fulani. Unapokurupuka kuna madhara yake kwani unaweza kutoa maamuzi kutokana na kusukumwa kihisia zaidi kuliko kuliangalia jambo kwa mtizamo wa ndani zaidi. Tumia muda kuangalia kwa umakini mambo yanaposhindikana na kuangalia mbadala wake katika hicho kilichoshindikana, usibishie kabla haujafanya uchunguzi wa ziada wa jambo hilo.

6. Inakubidi uachane na uzembe katika kufikiri na ufanyaji kazi wako. Uzembe kwa lugha rahisi ni kitendo cha wewe kutoweka muda na nguvu ya ziada kwa kile unachokifanya. Kama unataka kuwa mbunifu unahitaji muda wa kutosha wa hicho ambacho unataka kuongeza ubunifu kwa kutafutza mali ghafi na vitendea kazi, watu sahihi. Usiokote watu au vitu ambavyo si sahihi bila kuweka muda wa kutosha kujua kila kitu kitafanyika au kitu gani kinahitajika kwa usahihi zaidi.

NA BONGO 5

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>