Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Mavuji wanaojishughulisha na mradi wa kilimo cha umwagiliaji kwa matone umefadhiliwa na TASAF.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia chanzo cha maji ya mto Vuji yatakayotumika kumwagilia .
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua shamba lililofadhiliwa na TASAF
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaidiana kuweka tofali pamoja na Mkuuwa wilaya ya Kilwa Abdalla Ulega wakati wa kushiriki ujenzi wa nyumba ya mganga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendesha katapila wakati wa kushiriki ujenzi wa barabara ya Kwa Mkocho mpaka Kivinje.
Eneo linalovunwa chumvi Miina Kilwa Masoko.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki uvunaji wa chumvi Miina Kilwa Masoko
Ndugu Said Timamy (kulia) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye kiwanda cha chumvi cha Mishindo Salt Works kilichopo Miina Kilwa Masoko.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali baada ya kuwatembelea vijana wa kikundi cha ujasiriamali cha Majalala kilichopo Mnazi Mmoja Kilwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Mnazi mmoja Kilwa kabla ya kushiriki ujenzi wa ofisi ya tawi.
Katibu Mkuu wa CCM akishiriki ujenzi wa ofisi ya tawi Mnazi Mmoja Kilwa.
Hili ndo jiwe la msingi lililowekwa na Baba wa taifa mwaka 1987, jengo hili lilisimama mikaka mingi kutokana na matatizo ya umiliki wa kiwanja lakini sasa CCM imepata uhalali wa kumiliki eneo na ujenzi kuendelea.
Kikundi cha ngoma ya Ngongoti kikitumbuiza kabla ya kuanza kwa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakitumbuiza kabla ya kuanza kwa mkutano wa CCM mjini Kilwa Masoko.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Kilwa Masoko.
Sehemu ya Umati wa watu waliojitokeza kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa Bustani ya Mkapa Kilwa Masoko.
Mwananchi akishangilia jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kilwa Masoko kwenye uwanja wa Bustani ya Mkapa.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kilwa Masoko ambapo aliwaambia kuwa wapinzani hawasemi ukweli unaoendelea kwenye vyama vyao havisemi kama vimekufa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa akitoa salaam zake kwa wana CCM wa Kilwa Masoko kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM kuhutubia wananchi kwenye uwanja wa Bustani ya Mkapa.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Abdala Ulega akimpa mkono wa pongezi Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa baada ya kutoa darasa zuri kwa wananchi wa Kilwa Masoko.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kilwa Masoko ambapo aliwaambia watendaji wa serikali kutoa elimu ya kuwafahamisha wavuvi kabla ya kuchukua maamuzi ya kuchoma vifaa vyao vya kazi,pia aliwaambia wananchi hao kuwa Chama Cha Mapinduzi kitajirekebisha makosa yake na kuhakikisha kinashinda kwa kishindo kwenye chaguzi zijazo.
Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na kijana wa Kilwa baada ya kumaliza mkutano wake.
Wananchi wa Kilwa Masoko wakipiga picha na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Bustani ya Mkapa Kilwa Masoko.