Padfone
Linapokuja suala la soko la smartphone nchini Marekani, mara nyingi huwa ni mbio za farasi wawili tu, Apple na Samsung huku makampuni kama HTC na Motorola wakipigania soko kiduchu lililosalia.
Lakini hiyo inaweza kubadilika mwaka ujao pale kampuni ya Asus itakapoingiza sokoni PadFone yake nchini Marekani.
Vifaa hivyo vinavyotumia mfumo wa Android, vinadaiwa kuwa vya mapinduzi na vyenye nguvu ya kuwa mshindani kwenye soko la simu. PadFone inajumuisha tablet na smartphone pamoja.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Jina la phablet limeibuka siku hizi kuziita simu kama Galaxy Note III – kwamba ni ndogo mno kuwa tablet lakini pia ni kubwa mno kuwa smartphone. Lakini PadFone inaweza kuwa phablet ya ukweli.
Wanunuzi wanapata tablet na smartphone kwa wakati mmoja. PadFone ina ukubwa wa inchi 5 na processor kubwa na camera ya 13-megapixel. Kwa maneno mengine haiwezi kufananishwa na simu yoyote ya Android.
Badala ya kununua Galaxy S4 NA Galaxy Note 10.1 au iPhone 5s na iPad, wanunuaji wanaweza kununua , PadFone yenye vyote hivyo. Bei za PadFone nchini Marekani hazijatangazwa bado.