Kocha Andre Villa Boas ametimuliwa kazi ya kuinoa Tottenham Hotspur.
Kocha huyo raia wa Ureno ametimuliwa baada ya timu yake kupokea kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Liverpool iliyochezwa December 15, 2013 na pia mechi ya Tottenham alipofungwa na Man City mabao 6-0 iliyochezwa November 24, 2013 pia imekuwa sababu kubwa ya kutimuliwa kwa kocha huyo Mreno
Timu hiyo imekuwa na mwenendo wa ovyo ikiwa chini ya kocha huyo.
Pamoja na timu hiyo kufanya usajili uliogharimu mamilioni ya fedha, lakini haikuwa kali kama wengi walivyotarajia.