Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

BREAKING NEWS: MSIKITI WA MTAMBANI KINONDONI WAUNGUA TENA

$
0
0
 Sehemu ya Waumini wa Kiislam wakisaidiana  kupandisha mpira wa zima moto.


ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Habari zilizotufikia ni kwamba Msikiti wa Mtambani uliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam unateketea kwa moto hivi sasa. Hii ni mara ya pili msikiti huo kutetekea kwa moto baada ya kuungua Agosti 13 mwaka huu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura (wa pili kulia) akitoka katika Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam, ambapo moto ulizuka katika ghorofa ya pili katika Shule ya Sekondari ya Mivumoni.
 Sehemu ya Waumini wa Kiislam wakisaidiana  kupandisha mpira wa zima moto.
  Gari la Zima Moto likiwa limefika eneo la tukio
Shughuli ya Kuzima Moto ikiendelea.
Mashuhuda wakiwa kwenye eneo hilo

 Ulinzi mkali wa Polisi ulitawala katika eneo la Msikiti huo wa Mtambani kuhakikisha Usalama unakuwepo kwenye eneo hilo.

Mashuhuda wakiwa kwenye eneo hilo



Msikiti  wa  Mtambani uliopo Kinondoni jijini Dar es Saam uliungua kwa mara ya pili leo.  Msikiti huo ambao uliungua  mnamo Agosti 13, 2014 katika ghorofa yake ya juu na kuteketeza  eneo kubwa ambalo hadi sasa bado halijanza kufanyiwa  ukarabati.
Leo hii moto ambao inasemekana ulianza mmajira ya saa sita na nusu mchana   katika moja ya chumba ambacho wanafunzi wa kidato cha nne  wa kike wamekuwa wakipiga kambi ya kujisomea ikiwa ni katika maandalizi ya kukabiliana na mtihani wao wa taifa  utakaofanyika  baadaye mwaka huu.
 Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kanda ya Kinondoni Camilius Wambura  amethibitisha jambo hilo na kusema kuwa hadi wanafika eneo la tukio chanzo bado hakijafahamika, na kwamba chumba ambacho moto ulianzia ni cha wasichana ambamo  magodoro manne yameungua.
“Katika janga la moto uliounguza madarasa  mwezi uliopita Jeshi la Polisi iliunda  timu ambayo ilikuwa ikichunguza chanzo cha moto huo hivyo na sasa timu hiyohiyo itaendele na uchunguzi wake kwa kuunganisha matukio haya mawili” alisema Wambura.
Wakizungumza bila ya kutaja majina yao kina mama wa msikitini hapo wao walisema  kwamba “ sisi tulikuwa msikitini tunasoma qurani wakati tukivuta muda wa sala ya Ijumaa ndipo tuikasikia sauti za moto moto na kuona upande wa wanaume wakikimbia huku na kule kwa taharuki hivyo chanzo hasa cha moto sisi hatukijui.
Waumini wa msikiti huo walifanikiwa kuuzima moto huo na kusali swala ya Ijumaa kama kawaida. 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>