Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

UNAJUA NI KWANINI NI MUHIMU KUFURAHIA KAZI YAKO NA SIO KUFANYA KAMA UMELAZIMISHWA? SOMA HAPA UJITAMBUE

$
0
0

Nina furaha kupata kitu kisicho cha kawaida mwanzoni; namaanisha kwa nini mtu awe chanya na mwenye nguvu siku zote. Nilipigwa mshangao na shauku kubwa ninapoona watu wana furaha wakati wote.

Niimeelewa kuwa unatakiwa kuwa na mtizamo chanya hata unapotoa salamu, moja ya siri za ndani ni kuwa na mtizamo chanya, unapohisi vitu haviendi sawa usimwambie mtu vile unavyojihisi, badala yake mwambie unavyotaka kujisikia au matarajio yako ni nini katika hali hiyo. Kama unajibu ni vyema na salama, lakini usiruhusu hisia hasi kuharibu namna unavyotaka kujisikia vizuri ndani yako.
Ukijidhibiti jinsi unavyoongea na watu wengine kwa kutumia maneno yenye mtizamo chanya, itakusaidia kubadilika na hata hali yako kimawazo na kiakili itabadilika. Sio tu ni faida binafsi kwako bali utatambua matokeo ya mtizamo chanya utakao kuwa nao kwa watu wengine watatokea kukupenda na kutokuwa na mashaka wanapokuwa na wewe. Jaribu, kuwa na mtizamo chanya na furaha wakati wote mbele za watu usiruhusu hisia hasi au mtizamo hasi uharibu furaha yako.
Kuwa na Furaha ni jukumu lako binafsi ambalo litakusaidia kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, hivyo hupaswi kumtupia mtu lawama. Unapokuwa kazini kama hiyo kazi uliomba mwenyewe hivyo jukumu la kufurahi ni la kwako mwenyewe.

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Kwa Wastani waajiri wengi wananunua dhana za kazi kwa kuangalia ubora na umuhimu wake
Waajiri wanatarajia wafanyakazi kufanya kazi waliopewa.Wana matarajio kamili kwa wafanyakazi kwamba watafanya kazi kama ilivyotarajiwa,na kwahiyo huwa wanajigawanya katika idara kwa kuangalia kati yao uathirika/tatizo la mahali hapo ni nini. Kwahiyo kila mmoja atafanya vile inavyostahili.
Hivyo hivyo na wewe unahitaji kujua umuhimu wa wewe kuwa na furaha katika maisha yako au kazi yako ili kuleta matokeo bora zaidi kwenye utendaji wako.

Furaha katika kazi imekuwa ni moja ya tabia muhimu ambazo zinaongeza ufanisi wa hali ya juu na mafanikio katika taasisi husika.
Kuna mahusiano ya moja kwa moja kati ya furaha na kazi, ubunifu, uzalishaji, ari, na kuridhika kwako mahali ulipo. Vile vile kama unafanya kazi ya huduma kwa wateja furaha yako itaonekana kwa wateja wako hivyo kuvutiwa na huduma unayoitoa katika biashara hiyo.

Zingatia sana ucheshi ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu.
Kulingana na tamaduni zetu tumeambiwa kuwa kicheko, furaha,na kucheza ni kwa watoto, wasiona na uelewa na wasio na ujuzi.Hakuna kitakacho kuwa mbali na ukweli, moja kati ya vielekezo vya mwanzo vya magonjwa ya akili ni upotevu wa maana ya furaha katika kuwa hai wa mwanadamu. Kitu cha muhimu sana kukumbuka kupitia ni kutoendeleza ucheshi usiokuwa na maana au kufanya ujinga. Hivyo ni muhimu kwa kiongozi hata wafanyakazi. Katika uongozi tunajifunza kuwa wacheshi na sio kuwa mkali wakati wote bila sababu, ni vizuri kufurahi, lakini sio kuwa mjinga.

Mfano “Mama muuza mboga mboga alikuwa hataki kuniuzia mboga zake zote kwa sababu ya uhaba wa kimawazo”. Akafikiri akiuza zote na mapema ataenda kufanya nini? Badala ya kufikiri huyu mteja anaweza ku na matumizi makubwa, je kwanini nisiulize anahitaji kiasi gani kila siku au kila wiki? Je kwanini nisitengeneze mahusiano na wateja wangu na kufurahia ninachokifanya. Ujinga unaweza kukusababisha uonekane unafanya kitu kwa hasira au kutokuwa na uelewa wa kile unachokifanya kana kwamba umalazimishwa.
Ujinga ni umasikini ni janga na kama hatutabadilika vile tulivyo au vile tunafikiri,tutakuwa tu na kile tulicho kipata bila kufikiri zaidi ya hapo tulipo.

Na baada ya maongezi ya muda mrefu alikuwa tayari kujifunza na kubadilisha tabia yake
Mama mboga sio tu aliwasilisha mboga nzuri asubuhi na mapema kila wiki,pia alipiga simu kupata kujua wiki inayofuata kuna uhitaji wa kiasi gani. Hivi sasa ametengeneza orodha ya wateja wake wa kudumu wanaohitaji mboga kwa wiki na kujua namba ya wateja wake anao wasambazia mboga.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>