Vijana watanashati wa Skylight Band wakimsindikiza Sam Mapenzi (wa pili kuhsoto) kutoa burudani ya Live Music kwa mashabiki wa bendi hiyo Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam, huku usiku wa leo wataungana na mashabiki wake kusheherekea Birthday Mr. Jack's huku mlangoni wakipata SHOT za Jack Daniel's kusindikiza usiku huo.
Divas wa Skylight Band wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mary Lucos, igna Mbepera na Meneja wa Band Aneth Kushaba AK47 wakiwajibika.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Sony Masamba wa Skylight Band akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo huku akicheza "style" mpya ya bendi hiyo inayoitwa "FUNGA ZIPU" sambamba na Mary Lucos na Aneth Kushaba AK47.
Sehemu ya mashabiki wakisakata sebene la Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Mutu muzima Joniko Flower akipiga vocal na kupewa sapoti na Mary Lucos, Sony Masamba na Digna Mbepera.
Zipopo zilikunyumba.......ni moja ya Swaga za Skylight Band huku mashabiki nao hawakukubali kushindwa.
Ni raha iliyoje unapoanzisha kitu na mashabiki wako wakipenda kujifunza na kukicheza kama wewe....Skylight Band #Balsaaaa# ndio habari ya mujini.
Mpiga kinanda wa Skylight Band ambaye anahusika sana kunogesha muziki wa Live wa Skylight Band.
Huku burudani ikiendelea #WANAMANYOYA wakipata Ukodak kutoka kulia ni Joshua Ndege, The Big Boss Sebastiana Ndege, Rais wa Wanamanyoya Justine Ndege, Magaua pamoja na Eddievied.
Aneth Kushaba AK47 a.k.a Komando kipensi akipiga vocal za uhakika kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye uwanja wao wa nyumbani Thai Village ambapo leo patakuwa hapatoshi baada ya kukusanya mashabiki wapya kwenye NYAMA CHOMA FESTIVAL 2014 wikiendi iliyopita.
Hashimu Donode a.k.a Mzee wa Kiduku akiwajibika jukwaani na hisia kabisa.