Umesikia watu wakisema“wanajifunza kutakana na makosa” ni kweli kwamba kila ufahamu tunaoupata unatokana na makosa tuliyokwisha kufanya wakati fulani. Lakini utasema nini pale ambapo unafanya taaluma ambayo umekosea? Je unafikiri utapata muda wa kujifunza kutakana na kosa hilo? Inawezekana hilo ni kosa litakalogharimu maisha yako kwa kiasi kikubwa.
Amini usiamini unaweza kubadilisha kazi mara tatu au mara nne kwa mwaka na hali yako ya kifedha isiathirike.
Kama umetumia miaka mitano kusoma kitu kisicho sahihi halafu unataka kubadilisha lazima uathirike kwa namna moja ama nyingine. Ni bora ujue toka mwanzoni kuhusu taaluma unayoiendea kabla ya kufanya makosa makubwa.
Kwa sasa inawezekana unafanya kazi na umechanganyikiwa, huyu mwandishi anamaanisha nini? Je hata mimi nimepotea? Hebu fuatilia maswali matano hapa ili uweze kujua kama uko kwenye taaluma sahihi au la!
Haufurahii kazi yako
Pale ambapo unaridhika na kazi unayofanya ndipo ni rahisi kujua umefanikiwa vile kwenye taaluma hiyo, lasivyo hautakuwa umefanikiwa. Kuna watu huamua kufuata taaluma fulani kwasabu watu wengine ameona wamefanikiwa, huo ni ujinga. Ingawa unahitaji kuchagua taaluma kulingana na ujuzi ulionao vilevile na utu /hulka na tabia ulizonazo. Usifuate mkumbo kwenye taaluma mwisho wake utaishia kuvunjika moyo na kupata msongo wa mawazo.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Utendaji wako wa kazi hauendi Vizuri
Kitu kingine ambacho kinaonyesha uko katika taaluma sahihi ni utendaji wako wa kazi. Utendaji wako wa kazi unaokuwa vizuri na haukupi shida inawezekana kwa kiasi kikubwa uko mahala sahihi, hivyo bila kufanya juhudi hauwezi kwenda hatua ya juu. Ingawa kuna mashirika mengine hupandisha vyeo watu waliokaa muds mrefu kazini kitu ambacho sio sahihi. Kama utendaji wako wa kazi unashuka kila mara, inawezekana hauko sehemu sahihi hivyo fanya maamuzi ya msingi hapo.
Hujaridhika na Majukumu yako ya kazi
Hata kama umepandishwa cheo lakini majukumu ya kazi yako huyapendi au hujaridhika nayo inamaanisha uko kwenye taaluma ambayo si ya kwako. Kumbuka kuridhika na kazi pamoja na majukumu take ni kitu cha msingi kinachokusaidia kufanikiwa na kukujenga kitaaluma na ndipo utakapoonyesha umefanikiwa.
Una Msongo wa Mawazo au Kutojielewa
Msongo wa mawazo na kutojielewa ni vitu ambavyo huwapata sana watu ambao wanafanya kazi. Ingawa kazi ambayo inakupa msiongo wa mawazo mwingi inaathiri afya yako pole pole na inaweza kukusababishia kushindwa kufanya kazi wakati mwingine. Kama Msongo wa mawazo ni kitu kisichokoma kwenye taaluma uliyopo chukua tahadhari umepotea njia.
Unafikiria kuacha kazi na kurudi shule
Hili ni kosa kubwa ambalo wafanyakazi wengi hulifanya. Wengi huacha kazi kwa sababu hawawezi kusoma na kufanya kazi wakati mmoja, hiyo ni njia mbaya au maamuzi mabaya kama unataka kufanya taaluma sahihi. Kwa mtu kama huyu mfumo wa elimu umebadilika na sio kama zamani, siku hizi kuna vyuo vinatoa elimu kupitia njia ya mtandao.
Kwahiyo unahitaji kuchukua fursa ya mtandao na wakati huo huo unaendelea kupata uzoefu katika kazi unayofanya. Na vile vile elimu kwa njia ya mtandao ni kitu ambacho wengi wanaweza kufanya kwa sababu ya gharama kuwa chini ni urahisi wa kuendelea kusoma. Unapofuata hatua hizi hautapata shida dana ya kujua taaluma sahihi unayotaka kuichukua, kazi kwako. Unaruhusiwa kutoa mchango wako na namna ulivyopata taaluma sahihi kwa ajili yako.