Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

ZITTO: SINA UHUSIANO NA MWASITI WALA DIVA

$
0
0


Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe ameibuka na kukana kuwa na mahusiano na mtangazaji wa Clouds FM, Loveness ‘Diva’ pamoja na msanii wa muziki, Mwasiti.
Zitto alifunguka hayo juzi kupitia kipindi cha Mkasi cha EATV ambapo alikanusha kuwa na uhusiano wowote wa mapenzi na mastaa hao licha ya kudaiwa kutungiwa wimbo na Diva.

“Mh! Kama yeye amenitungia wimbo sijui lakini mimi sina uhusiano naye wowote wa kimapenzi,” alisema Zitto.
Katika hatua nyingine Zitto alizungumzia pia tetesi kuwa ana uhusiano mwingine na staa wa Bongo Fleva, Mwasiti Almasi na kudai hakuna ukweli wowote.
“Naumia sana kusikia wakinisema na Mwasiti wakati yule ni dada yangu na mbaya zaidi ni mtu ambaye mara kwa mara nimekuwa nikimsaidia katika shughuli zake za muziki, hakuna kitu kingine zaidi ya ukaka na udada,” alisema Zitto.
Aidha, mheshimiwa huyo mbali na kungumzia mikakati yake ya kisiasa katika kipindi hicho, aliweka bayana kuwa ni baba wa mtoto mmoja kwa mchumba wake aliyemtaja kwa jina moja la Jack na wanamlea mtoto wao vizuri lakini suala la ndoa bado halijatimia.

Source:GPL

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles