Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela
--------------------------------------------------
Na Nathan Mtega,Songea
JESHI la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia askari wake wawili kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumpiga risasi mwendesha piki piki aliyejulikana kwa jina la Salgo Ndunguru(22) mkazi wa Ruvuma mjini Songea.
Akizungumza kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela amesema tukio hilo limetokea Agosti 26 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea ambapo askari polisi wawili PC Waziri mwenye namba G 5075 na PC Ayoub mwenye namba G 9800 wakiwa doria na piki piki ya polisi yenye namba za usajili PT 1250 CR aina ya Yamaha CC 250 katika eneo hilo la Kombezi walimjeruhi mwendesha piki piki huyo kwa kumpiga risasi.
Amesema mwendesha piki piki huyo alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na askari PC Waziri katika harakati za kuinsuru silaha hiyo iliyokuwa imebebwa na askari mwenzake PC Ayoub ambaye alizingirwa na baadhi ya waendesha piki piki wakiongozwa na mwendesha piki piki aliyejulikans kwa jina moja la Agrey ambaye alidai kuwa yeye ndiye mmiliki wa piki piki iliyokamatwa na askari hao ikiwa imebeba mzigo wa majiko.
Amesema mwendesha piki piki huyo alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na askari PC Waziri katika harakati za kuinsuru silaha hiyo iliyokuwa imebebwa na askari mwenzake PC Ayoub ambaye alizingirwa na baadhi ya waendesha piki piki wakiongozwa na mwendesha piki piki aliyejulikans kwa jina moja la Agrey ambaye alidai kuwa yeye ndiye mmiliki wa piki piki iliyokamatwa na askari hao ikiwa imebeba mzigo wa majiko.
Ameitaja piki piki iliyokuwa ikiendeshwa na majeruhi huyo kuwa ni aina ya San Lug yenye namba za usajili T 757 CUD ambapo baada ya mwendesha piki piki huyo kukamtwa alimpigia simu mdhamini wake Agrey alipofika alisababisha mkusanyiko mkubwa wa waendesha piki piki maarufu kama Yebo yebo ambao walianza kuwarushia mawe askari hao huku majeruhi akiwa ameshika mtutu wa bunduki iliyokuwa imebebwa na askari PC Ayoub ndipo askari PC Waziri katika kuinusuru silaha isiporwe alimpiga risasi majeruhi kwenye kiganja cha mkono wa kushoto na risasi hiyo kumjeruhi sehemu mbili ambazo ni kiganja cha mkono wa kushoto na paja la mguu wa kushoto.
Amesema majeruhi amelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea kwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri na katika vurugu hizo zilizodumu kwa muda wa nusu saa kabla ya kutulizwa na kikundi cha askari maalumu kilichowahi na kutuliza vurugu hizo kwa kutumia nguvu kidogo hali ikarejea kuwa shwari na hakuna madhara zaidi yaliyojitokeza.
Aidha kamanda Msikhela amesema uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo unaendelea na hatua zitachukuliwa dhidi ya wahusika watakaothibitika na ametoa wito kwa waendesha piki piki kuacha tabia ya kushabikia vurugu ambazo hazina tija na kuwa chanzo cha kusababisha migogoro isiyokuwa na maana na kusababisha madhara kwa jamii.
Amewataka waendesha piki piki kufuata taratibu zilizopo ikiwa ni pamoja na kuwasilisha malalamiko yao kwa viongozi husika kwa kupitia viongozi wao ili yaweze kufanyiwa kazi amewataka wananchi mkoani Ruvuma kuwa watulivu na kuendelea na shughuli zao bila hofu yoyote kwani jeshi la polisi liko imara kulinda mali na maisha yao.