Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOANI DODOMA KUHUSU MAPIGANO YA WANAKIJIJI WILAYA YA CHEMBA MKOANI DODOMA.

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP

Na: Peter Simon wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawasaka watu wawili kwa tuhuma za kuchochea mapigano yaliyopelekea mtu mmoja kuuawa na wengine saba (7) kujeruhiwa ambao wanapatiwa matibabu katika Zahanati ya Kwamtoro Wilayani Chemba Mkoa wa Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema mapigano hayo yametokea tarehe 11/08/2014 majira ya 20:00 katika kijiji cha Bubutole Mbuyuni Kata na Tarafa ya Farkwa Wilaya ya Chemba baiana ya wanakijiji wa asili wa eneo hilo na wasukuma ambao wamechukuliwa kama wageni jambo ambalo ni kinyume na sheia za nchi.

Kamanda MISIME amesema aliyeuawa katika mapigano hayo kwa kuchomwa mkuki kifuani upande wa kulia ni DOGANI S/O LUPONDIJE mwenye miaka 48, Msukuma na Mkazi wa Bubutole Wilayani humo.

Aidha Kamanda MISIME amesema Jeshi la Polisi Mkao wa Dodoma linawasaka ADAMU S/O SWALEHE Msandawe na ALLY S/O RAMADHANI ambao wote ni wakazi wa kijiji cha Bubutole na Mkoani Arusha kwani ushahidi unaonyesha ndio waliokuwa wanachochea vurugu hizo zilizopelekea mauaji.

Amesema chanzo cha mapigano hayo ni kile kinachodaiwa kuwa kunamradi wa upimaji ardhi katika kijiji hicho unaoendelea kwaajili ya kuhamisha watu ili lijengwe bwawa. Hivyo wenyeji wanadai itakuwaje walipwe fidia wageni ambao ni wasukuma.

Kamanda MSIME ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi na watambue kila raia ana haki ya kuishi popote ilimradi havunji sheria za nchi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>