Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

BI. VAILET MAKAZI WA MTANANA WILAYANI KONGWA AOMBA MSAADA ILI AKAFANYIWE UPASUAJI

$
0
0
Na John Banda,Kongwa.

Bi Vailet Sekwao (40) mkazi wa kijiji cha Mtanana Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma, anaomba msaada wa kifedha kiasi cha shilingi million mbili (2) ili aweze kufanyiwa upasuaji wa jicho lake ambalo lina uvimbe.

Akizungumza na mwandishi wetu katika kijiji cha Mtanana alisema kuwa anaomba msaada huo ili umwezeshe kugharimikia gharama za kumfikisha katika Hospitali ya Mhimbili na kufanyiwa upasuaji  wa uvimbe ulioko kwenye jicho.

Sekwao alisema kuwa uvimbe huo ambao ulinza kama kipele pembezoni mwa jicho hilo mwaka 2013,uliazidi kuongezeka na kufikia hatua ya kuvimba na kulifanya jicho hilo kutokuwa na uwezo wa kuona.

Alisema pamoja na juhudi za kwenda hospitali mbalimbali ikiwemo ya Mvumi, hali jicho hilo limezidi kuvimba na waatalam wamenishauri nikafanyiwe upasuaji kwa hatua iliyofikia.

“Kwa kweli ninapata maumivu makali sana hivyo ninawaomba wasamaria wema,taasisi na mashirika kunisaidia kiasi hicho cha fedha ikibidi hata kama kuna uwezekano wa kuweza kunitibu mimi nitakuwa tayari tu ,kwani hivi sasa nimeuza kila kitu ikiwemo nyumba,shamba na kiwanja,kwa ajili ya kupata fedha za kujitibu”alisema.

Bi Sekwao hata hivyo alisema kwa wale wote watakaogunswa na kilio changu kwa lengo la kunisaidia ninawaomba watumie namba zifuatazo za simu 068752216007881077530682400989 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>