Utafiti mpya umebaini kuwa wafanyakazi wanaotumia muda mwingi kwenye ofisi isiyokuwa na madirisha – au kwenye ofisi ambazo hazipati mwanga wa kutosha kutoka nje, hukosa usingizi kwa walau dakika 46 kila usiku.
Wale wanaokaa karibu na dirisha wamebainika kutokuwa na usingizi wa kushtuka na maisha bora zaidi kuliko wale wasiopata mwanga wa kutosha. Utafiti huo uliochapishwa kwenye Journal of Clinical Sleep Medicine, umedai kuwa ofisi zilizotengenezwa vizuri huboresha afya ya kimwili na kiakili ya wafanyakazi.
Watu wengi wanaofanya kazi za ofisi mijini wanapata usingizi hafifu ambapo msongo wa mawazo, matumizi ya computer na kupeleka kazi za ofisi nyumbani vinadaiwa kuwa ni sababu kubwa.
Hata hivyo malipo ya kukosa usingizi hayaashi katika kuwa na mood mbaya ama kupunguza umakini muda wa mchana bali wale wanaopata usingizi kidogo wanaweza kupata matatizo ya kiafya kama kunenepa, kisukari na ugonjwa wa moyo.
Kupata mwanga asili mara kwa mara ni muhimu kwa kusaidia ‘circadian rhythm’ – saa katika mwili wa binadamu inayosimamia ratiba zetu za kulala na kuamka.
Utafiti huo ulifanywa kwa pamoja na vyuo vikuu vya Illinois, Northwestern University in Chicago na Hwa-Hsia Institute of Technology cha Taiwan.