Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Uchina, Bw. Jiang Zhigang (Katikati) akiongoza mjadala wakati wa majadiliano na na Uongozi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (Hawapo pichani) juu ya uwezekano wa Benki hiyo kufadhili baadhi miradi ya maendeleo nchini.
Naibu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mashirikiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe (Kulia) akibadilisha mawazo na Ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Uchina (Hawapo pichani) wakati walipotembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango .
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Uchina, Bw. Jiang Zhigang (Katikati) akisisitiza jambo wakati walipokuwa na mazungumzo na Uongozi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Kushoto ni Mtafiti Kutoka ‘State Information Center’, Bw. Chen Qiang na Kulia ni Bw. Zhao Bingjie, Mhandisi Mwandamizi kutoka ‘Railway Third Survey and Design Institute Group’.
Naibu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mashirikiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe (Kushoto) akiwasilisha Mada ya Hali ya Uchumi wa Tanzania wakati Ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Uchina ulipoitembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Mwenyekiti wa Majadiliano kati ya Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Benki ya Maendeleo ya Uchina, Bw. Maduka Paul Kessy (Wapili Kulia) akizungumza wakati wa Majadiliano. Kulia ni Naibu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mashirikiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe. Wengine pichani ni wajumbe wa majadiliano, Bi. Martha Luanda (Kushoto) kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Bw. Medard Ngaiza (Wapili Kushoto), kutoka Dawati la Uchina, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Wakili wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Wakili Nyanzala Nkinga (Katikati) akifafanua jambo kwa mmoja kati ya wajumbe wa majadiliano, Bibi Martha Luanda (Kulia). Kushoto ni Bi. Gloria Ngowi.
Picha na Saidi Mkabakuli
*Yazungumzia uwezekano wa kugharamia utekelezaji wa miradi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025
Na Saidi Mkabakuli
Ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Uchina umetembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kwa minajili ya kuja kujadiliana juu ya uwezekano wa kugharamia miradi ya maendeleo kwa upande wa barabara, kilimo na nishati ili kuiwezesha Tanzania kufikia lengo lake la kuwa nchi ya uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.
Ugeni huo unaongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Jiang Zhigang utatembelea wizara mama zinazosimamia miradi itakayogharamiwa na Benki hiyo ambazo ni pamoja na Wizara ya Kilimo, Wizara ya Uchukuzi na Wizara Nishati na Madini.
“Tumekuja Tanzania kwa ajili ya kukagua na kujionea maendeleo ya sekta za kipaumbele ambazo tutagharamia ili kupata uelewa wa gharama halisi ya miradi hiyo,” alisema Bw. Zhigang.
Kwa mujibu wa makubaliano ya awali yaliyofanyika mwezi Julai, 2012 kati ya taasisi hizi mbili, Tume ya Mipango imekubali kupatiwa utaalamu elekezi kwenye maeneo hayo wenye lengo la kukuza ushirikiano wa kihistoria baina ya nchi hizo.
Wakati huo huo, imebainika kuwa Tanzania imekuwa kinara katika kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi miongoni mwa nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara kutoka asilimia 18 ya Pato la Taifa (GDP) kwa mwaka 2002 hadi kufikia asilimia 34 kwa mwaka 2013.
Hayo yamewekwa wazi na Naibu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mashirikiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe wakati akiwasilisha mada ya Hali ya Uchumi wa Tanzania wakati Ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Uchina ulipoitembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
“Tunajitahidi kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi, kwa mfano, mwaka 2003 tuliweza kuvutia uwekezaji kutoka nje ‘Foreign Direct Investment (FDI)’ wa jumla ya Shilingi za Kimarekani milioni 308.2, na mwa 2013 zilifikia Shilingi za Kimarekani milioni 1,872.4,” aliongeza.