Watu wengi wanaposhindwa jambo au mambo fulani huwa hatuombi msaada ili tuweze kusaidiwa pale ambapo tuna tatizo au kushindwa. Tunaogopa kuonekana kwamba kumbe hatujui kulingana na jinsi watu wanatufahamu na kutuheshimu.
Kama hujui kitu ni hujui hakuna namna ambavyo unaweza kukwepa jambo hilo hata kama una umaarufu kiasi gani. Kama unataka watu wakuheshimu kwa mambo unayoyajua wajue unajua na usiyoyajua wajue huyajui kwa kufanya hivyo unatengeneza mlango wa watu wengine kukusaidia na kushirikiana na wewe.
Hakuna Binadamu ambaye anajua kila kitu hata kama ni maarufu kiasi gani, kitu cha kujiuliza kama sijui jambo hili nifanyeje? Hebu tuangalie mambo yanayofanya watu kutoomba msaada kama wanashida ya kutojua kitu fulani;
Hawataki kuwa Mzigo; Ukweli ni kwamba huwezi kujua kila kitu kwahiyo kila mtu anahitaji msaada wa kitu fulani. Kama unaonekana ni mzigo kwa mtu fulani hakuna kosa juu yako, kosa au tatizo ni pale unaposhindwa kudhibiti mipaka yako. Kuna watu wako maofisi na kuna vitu hawajui na wanaendelea kung’ang’ana kana kwamba wanajua wanachokifanya kumbe hawajui. Hawataki kuonekana ni mzigo kwa watu wengine.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wengine huogopa mtu akikataa; Hautabadilika hata kama mtu akisema hapana sitoweza kukusaidia, tatizo lako litabaki palepale na kama akikubali inamaanisha utapata ufumbuzi wa tatizo lako. Hivyo basi unahitaji kufanya utafiti wa tatizo lako au wa kitu ambacho hukijui na uje nani anaweza kukusaidia kiushauri hata ufumbuzi wa moja kwa moja. Inakubidi ujaribu na usiogope kuuliza usichojua.
Wengine hawataki kuonekana wajinga au hawawezi;
kuuliza si ujinga kama hujui unapouliza inakusaidia upate kuelewa. Kwahiyo kama wewe huwezi ruhusu watu wengine wakusaidie kufanya na mwisho wa siku kitu kitafanyika na kama huna muda kitu kitafanyika ingawa huna huo muda.Watu wenye hekima hutafuta hekima kwa watu wenye uzoefu kuliko wao katika jambo fulani na huomba msaada.
Utamaduni au tabia ya Kabila na Mahali alipotoka. Hata kama unatoka katika makabila au tamaduni za watu ambao wamejijengea kwamba wao wanajua kila kitu hata kama hawajui, ni wakati wa kufanya tofauti na tamaduni na jeuri za makabila yetu. kama hujui ni hujui hivyo unahitaji mtu akufundishe au akusaidie kile usichokijua hivyo ndio namna ambavyo unaweza kusonga mbele na kufanya vitu na watu wengine.
Ila kujifanya unajua wakati hujui ni ujinga mtupu. Hivyo kuuliza ni namna ya kujifunza ili uweze kufikia hatua ya kujua jambo, hutakiwi kuwa na aibu au woga unapotafuta kujua jambo fulani. tafuta watu unao waamini ambao watakusaidia uweze kujua na kujifunza vitu tofauti tofauti kutokana na uzofu wao na mazingira waliopitia.