MAHAKAMA ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imewahukumu walimu watatu na mfanyabiashara mmoja kifungo cha miaka 579 jela kwa kupatikana na hatia ya kuiba fedha za shule Sh milioni 21. Walimu hao ni wa shule ya Msingi Tukoma katika Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele na mfanyabiashara wa mjini Mpanda.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Chiganga Ntengwa baada ya mahakama kuwatia hatiani kwa makosa 64.
Washitakiwa hao ni mwalimu Joel Mwakyusa (37) mkazi wa Kawajense aliyehukumiwa kifungo cha miaka 255 kwa kupatikana na makosa 40 ya wizi wa fedha.
Mwingine ni mwalimu mkuu wa shule hiyo, Lenatus Ngalo (50) mkazi wa Nsemlwa aliyefungwa 148 kwa kupatikana na hatia ya makosa 38 na mwalimu
Joachimu Katabi (39) mkazi wa Majengo aliyehukumiwa kifungo cha miaka 143 .
Aliyefungwa mwingine ni mfanyabiashara Fredilik Mlenje (50) mkazi wa Nsemulwa ambaye akaunti yake ilitumika kuiba fedha hizo.
Washitakiwa hao walidaiwa kutenda kosa hilo mwaka 2009 kwa kugushi nyaraka zilizowawezesha kuiba fedha hizo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Chiganga Ntengwa aliwataka washitakiwa watakapomaliza kifungo wote kwa pamoja warejeshe fedha hizo
RAI