Rais wa Fifa Sepp Blatter amesema ameshangazwa kuwa Lionel Messi alishinda tuzo ya mchezaji bora – Golden Ball Award- katika Kombe la Dunia.
Messi, 27, alitajwa kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo licha ya timu yake Argentina kufungwa 1-0 na Ujerumani kwenye mchezo wa fainali Jumapili mjini Rio de Janeiro.
“Nilishangazwa kidogo nilipoona Messi anakuja kupokea tuzo ya mchezaji bora,” amesema Blatter, ambaye alikabidhi tuzo hiyo.
Naye mkongwe wa Argentina Diego Maradona ameita tuzo hiyo kuwa “si haki”.
Tuzo ya mpira wa dhahabu ya mchezaji bora na ya kipa bora hupigiwa kura na kamati ya ufundi ya Fifa inayojumuisha kamati ya wachambuzi.
Tuzo ya mchezaji chipukizi ilikwenda kwa Paul Pogba wa Ufaransa.