MBUNGE waviti maalumu mkoa wa Mara kupitia vijana Ester Bulaya(CCM) ametoa msaada wa mashuka 200 kwenye kituo cha afya cha Manyamanyama kilichopo wilayani Bunda ikiwa ni jitihada za kuchangia kituo hicho kilicho kwenye mchakato wa kutangazwa hospitali ya Wilaya. Akikabidhi msaada huo kwa wagonjwa waliokuwa wamelazwa kwenye wodi ya Wanawake,Watoto naWanaume,Bulaya alisema akiwa kama mkazi wa Manyamanyama,Bunda na kiongozi anayeguswa namasuala ya kijamii aliguswa na uhaba wa mashuka kwenye kituo hicho na kuamua kuchangia sehemu ya upungufu. Alisema alipotembelea kituo hicho kwa siku za nyuma alipewa taarifa ya upungufu mkubwa wa mashuka kwenye kituo hicho na kupelekea wagonjwa kulala bila kijifuni wala kutandika na kuamua kujibana katika sehemu ya kipato chake na kununua mashuka 200 kwa kuanzia. Mbunge huyo ambaye mara kadhaa amekuwa akizungumzia kituo hicho cha afya bungeni na namna ambavyo licha ya kuhudumia wangonjwa wengi kutokana na kuwa jirani na barabara kuu kuiomba Serikali kukamilisha mapema mchakato wa kuitangaza kuwa hospitali ya Wilaya ili iweze kupata mahitaji stahiki na kuwahudumia wagonjwa wanaofika kwenye kituo hicho. Alisema mashuka hayo 200 aliyotoa kwa namna moja yatasaidia kupunguza changamoto ya wagonjwa kupatwa na baridi na hata kutandika kwenye vitanda na pale atakapopata nafasi ataendelea kuchangia mahitaji mbalimbali yanayohitaji kakwenye kituo hicho ikiwa ni pamoja na vifaa tiba,madawa na kubwa ni kuhakikisha unazungushwa uzio ili kuzuia watu kuvamia maeneo ya hospitali. Kutoka na namchakato wa kupandishwa hadhi kituo hicho na kuwa hospitali ya Wilaya,Bulaya aliiomba Serikali kufanya jitihada za makusudi kukipa hadhi kituo hicho na kuwa hospitali kutokana na kutoa huduma muhimu licha ya changamoto ambazo zipo kwenye kituo. Akizungumzia msaada uliotolewa na Ester Bulaya,Mganga wa Wilaya ya Bunda Charles Mkombe alisema msaada alioutoa mbunge huyo umekuja wakati muafaka ambapo kituo hicho cha afya kinakabiliwa na uhaba wa mashuka 640 ili kukidhi haja. Alisema msaada huo umepunguz upungufu mkubwa uliokuwepo na kumshukuru Mbunge huyo kwa kuwa na moyo wakujali mahitaji hususani ya wagonjwa wanaofika na kulazwa kwenye kituo hicho cha afya ambacho kinatumiwa na watu wengi. Mkombe alisema mashuka ni moja ya changamoto kubwa waliokuwa nayo licha ya kuwepo na changamoto nyingine ikiwemo kutukuwa na uzio wa kuzunguka kituo hicho cha Manyamanyama na kupelekea baadhi ya watu kuvamia maeneo ya hospitali na kushukuru kauli ya Bulaya kuonyesha utayari wa kusaidia kuzungushwa uzio huo. Baadhi ya wagonjwa waliokuwa wamelazwa kwenye wodi na kupokea msaada wamashuka hayo,walimshukuru Mbunge huyo kwa kuwa walikuwa wakipata tabu sana hususani nyakati za usiku kwa kushikwa na baridi kutokana na kukosa mashuka ya kujifunika. |