Waziri wa ujenzi Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa iramba katika jimbo la mwibara kabla ya kuzindua kivuko cha mv. mara chenye uwezo wa kubeba tani 25 yani magari manne na abiria 50
Waziri wa ujenzi Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli katikati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kivuko kipya cha MV Mara kitakachotoa huduma kati ya maeneo ya iramba bunda na majita musoma vijijini. kutoka kushoto ni kaimu mkuu wa mkoa wa Mara Mhandisi Evarist Ndikilo akifatiwa na mbunge wa jimbo la Mwibara Alphaxad Kangi Lugora, wengine kutoka kulia ni katibu mkuu wa wizara ya ujenzi mhandishi Mussa Iyombe akifatiwa na mbunge wa Musoma vijijini Nimrod Mkono pamoja na mwenyekiti wa CCM mkoa wa mara Christopher Sanya.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Waziri wa ujenzi Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akibonyeza kitufe cha kivuko cha MV Mara kuashiria kukizindua rasmi kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kati ya maeneo ya Iramba na Majita katika wilaya mbili za Bunda na Musoma vijijini
Waziri wa ujenzi, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akipungia wakazi wa Mwibara mara baada ya kufungua kivuko cha MV Mara
Picha ya kivuko kipya cha MV Mara kama kinavyoonekana katika picha kabla ya kufunguliwa
Waziri wa ujenzi Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi za kimila kutoka kwa wenyeji wa bunda za kumtambua kuwa mkazi wa mji huo kwa kimila.
Waziri wa ujenzi Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa katibu mkuu wa wizara ya ujenzi mhandisi mussa iyombe kushoto huku mwenyekiti wa bodi ya Temesa Herbert Mrango pamoja na mtendaji mkuu wa Temesa mama Marcelina Magessa wakisikiliza kwa makini
Waziri wa ujenzi Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia na wanachama wapya wa chama cha mapinduzi (CCM) walioamua kujiunga na chama hicho mara baada ya waziri magufuli kumaliza kuhutubia mkutano.
Waziri wa ujenzi Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mwenyekiti wa bodi ya Temesa balozi Herbert Mrango huku mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono aliyessimama kulia na mbunge wa Mwibara Kangi Lugora wakwaanza kushoto wakiangalia
Baadhi ya wakazi wa Iramba katika jimbo la Mwibara wakiwa wamepanda juu ya miti ili kumshuhudia Waziri wa ujenzi Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya uzinduzi wa kivuko hicho
Picha ya boti ambayo ilikuwa ikitumika awali kuvusha watu kati ya Majita na Iramba kwa gharama ya shilingi 2000/=