Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Sophia Simba akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa baraza kuu la umoja huo lilipokutana juzi kwa ajili ya kikao cha kawaida cha mwaka kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Makao makuu Dodoma.
Katibu Mkuu wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Anna Makillagi akisoma agenda za mkutano wa Baraza la kawaida la umojahuo mbele ya wajumbe waliokusanyika katika ukumbi mkoani Dodoma.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakiwa katika ukumbi wa mikutano Dodoma walikutana kwa ajili ya kikao cha kawaida kilichofanyika juzi.
Na John Banda, Dodoma
BARAZA kuu la Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) limekemea vikali kuhusu matendo ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia wanaofanyiwa wanawake na watoto vinavyoendelea kutokea hapa nchini na mikoa ya kanda ya ziwa ambayo ndiyo inayoongoza kwa matukio hayo.
Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa UWT Amina Makillagi mara baada kumaliza kikao cha Baraza kuu la kawaida kilichokutana katika ukumbi wa mikutano wa White House uliopo CCM makao makuu Dodoma alipozungumza na waandishi wa Habari.
Alisema Baraza hilo limelaani vikali matukio yote ya mauaji ya wanawake, watoto na walevumi kwa ajili ya visingizio mbalimbali vikiwemo vya imani za kishirikina. Aidha Makillagi alisema kuwa mikoa iliyokithili kwa vitondo hivyo ni ile ya mikoa ya kanda ya ziwa ikiwemo ya Geita, Simiyu, Shinyanga na
Mwanza , pia mauaji ya walemavu wa ngozi na ukatili wa watoto yanayotokea sasa katika mikoa mingi hapa nchini. ‘’Vitendo hivyo viachwe mara moja maana kwa kutokana na visingizio mambo ya kishirikina yamekatisha maisha ya watu wengi wasio na hatia bila sababu, mamraka zote zinazohusika zihakikishe zinafanya kazi yake kikamilifu ili kuzuia uhalifu wa kutisha unaoendelea nchini’’, alisema
Aidha alisema kuwa Baraza la umoja huo liliwapongeza wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuunga mkono na kupitisha Bajeti ya serikali ya mwaka 2014/15 iliyolenga kuboresha maslahi ya mwananchi wa kawaida.
Aliongeza kuwa Baraza kuu hilo limeiomba serikali kutafuta fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya huduma za jamii kama vile umeme, maji, afya na mingineyo kama ilivyopitishwa na Bunge. ‘’Miradi ya kijamii kama umeme, maji na afya ni muhimu sana kwani ikikosekana wanaopata tabu ni wanawake na watoto ambao idadi yao ni kubwa kuliko wanaume’’, alisema Makilllagi.