Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akikagua nguzo zilizojengwa kwa
lengo la kuongeza uimara kwenye jengo la zahanati ya kijiji cha Mkonze Manispaa ya Dodoma lililokuwa limeathiriwa na nyufa kwenye baadhi ya kuta na kusababisha rasilimali hiyo ya serikali isitumike kutoa huduma kwa wananchi kwa sababu za kiusalama, Mkuu huyo wa Mkoa alifanya ziara hiyo Julai 3.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (katikati) akizungumza na baadhi ya Viongozi wa kijiji cha Mkonze, wajumbe wa kamati ya Afya kijijini hapo na baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Dodoma Julai 3 wakati alipotembelea zahanati ya Kijij hiko kukagua ukarabati wa jengo la zahanati ya kijiji lililokuwa limeathiriwa na nyufa kwenye baadhi ya kuta na kusababisha rasilimali hiyo ya serikali isitumike kutoa huduma kwa wananchi kwa sababu za kiusalama.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Jengo la zahanati ya kijiji cha Mkonze Manispaa ya Dodoma likiwa limeanza kujengewa nguzo kwenye kuta kwa lengo la kuliongezea uimara, Jengo hilo lililokuwa limeathiriwa na nyufa kwenye baadhi ya kuta na kusababisha rasilimali hiyo ya serikali isitumike kutoa huduma kwa wananchi kwa sababu za kiusalama.
Jengo la zahanati ya kijiji cha Mkonze Manispaa ya Dodoma ambalo lilikuwa limeathiriwa na nyufa kwenye baadhi ya kuta na kusababisha rasilimali hiyo ya serikali isitumike kutoa huduma kwa wananchi kwa sababu za kiusalama kwa sasa linafanyiwa ukarabati kwa kuanzia na kujengewa nguzo ili kulipa uimara na kuondoa mapungufu yaliyojitokeza ili jengo hilo lianze kutoa huduma.
Na John Banda, Dodoma
Mkuu wa Mkoa Dkt. Rehema Nchimbi amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuhakikisha anatoa kipaumbele cha mradi wa ujenzi wa zahanati ya Mkonze na kuhakikisha ukarabati wa jengo hilo unakamilika mara moja ili ianze kutoa huduma kwa wananchi.
Nchimbi alitoa agizo hilo baada ya kutembelea katika kjiji hicho cha Mkonze kilichopo Manispaa ya Dodoma na kujionea zahanati hiyo ilivyojengwa chini ya kiwango na kuamuru ukarabati ufanyike kitaaramu.
Alisema Mkurugenzi wa manispaa na timu yake wahakikishe wanatoa kipaumbele katika marekebisho ya ujenzi wa jingo hilo ambalo kuta zake zimeweka nyufa kabla hata ya kuanza kutumika. Alisema mradi huo unaonyesha kulikuwa na hali ya kulegalega kwenye utekelezaji na usimamizi wa ujenzi wa jingo hilo na hata wataaramu hawakufanya kazi yao ipasavyo ndiyo maana imejitokeza athari kama hizo.
Awali akisoma Risala kwa niaba ya wananchi Yusufu Jacob aliulalamikia usimamizi mbovu wa utekelezaji wa mradi huo hali ilisababisha changamoto hizo zinazochelewesha huduma kwa wananchi ambao wamekuwa wakifuata huduma za afya mjini kwa umbali mrefu hali inayowasababishia adha kubwa.
Ikumbukwe kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliwahi kutembelea Mradi huo mapema mwezi Machi mwaka huu na kujionea dosari hizo kwenye jengo hilo na kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa Dodoma na Timu yake ya Watendaji kulifanyia haraka ukarabati jengo hilo lianze kutoa huduma lakini aliporudi Mwezi Juni kuangalia utekelezaji wa maelekezo yake alikuta hali isiyoridhisha na kuagiza lisifunguliwe mpaka litakapokamilika. hiyo kujitokeza ujenzi huowa zahanati unaonekana haukuwa na usimamizi.