Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

TUME YA UCHAGUZI YA TAIFA YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI MKOANI DODOMA

$
0
0
 Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Tume ya uchaguzi ya Taifa Oigenia Mpanduji akitoa ufafanuzi wa jambo alipokuwa akitoa mada kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma kuhusu, Maandalizi ya Maboresho ya Daftari la kudumu wapiga kura kwa kutumia Teknolojia ya Biometric Voter Registration (BVR)  leo.
 Jaji Mkuu Mstaafu wa Nzanzibar ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa Uchaguzi  Mhe. Hamid Mohamoud Hamid akifungua Mafunzo kwa waandishi wa Habari wa mkoa wa Dodoma kuhusu Maboresho ya kudumu ya Daftari la wapiga kura iliyotolewa na Tume ya Taifa ya UchaguziKushoto Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Tume hiyo Oigenia Mpanduji,. kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Mhandisi Lusako Kilembe.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliopo mkoa wa Dodoma wakiwa katika ukumbi wa manispaa kufuatili semina iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu Maboresho ya kudumu ya Daftari la wapiga kura.

Na JOHN Banda,Daftari La kudumu la wapiga kura,Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Sera na Mipango wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Oigenia Mpanduji amesema kuwa changamoto zilizojitokeza katika awamu ya pili ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Optical Mark Recognition (OMR) na nyingine ndizo zimeisukuma Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufikia  kutumia Teknolojia itakayosaidia kuondoa changamoto hizo.
 
Akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya Biometric Voter Registration(BVR) katika Mkutano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na waandishi wa habari iliyofanyika Mjini hapa,Mpanduji alisema changamoto hizo zilisababisha daftari kulalamikiwa na wadau mbalimbali wa uchaguzi kwa kuhoji usahihi wake na hvyo kutotumika kwa baadhi ya wadau.
 
Mpanduji alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na kuwapo kwa majina ya watu waliofariki katika daftari,majina ya wapiga kura kutokuonekana kwenye daftari siku ya kupiga kura wakati walijiandikisha na wana kadi zao za kupigia kura,na kushindwa kurekebisha taarifa za waliotaka kurekebisha taarifa zao au kumhamisha  endapo mpiga kura huyo amehamia  sehemu nyingine .
 
“Katika awamu hii teknolojia itakayotumika  ni Biometric Voter Registration (BVR) ambapo alama zitakazochukuliwa kutoka kwa mpiga kura ni alama za vidole vyote kumi,picha na saini mpiga ya  kura”alisema Mpanduji.
 
Akijibu swali kuhusu   wafungwa kupiga kura katika uchaguzi Mpanduji alisema kuwa wafungwa hawaruhusiwi kupiga kura kwa sheria ya sasa.
 
“Kwa sheria ya sasa na taratibu tulizonazo wafungwa hawaruhusiwi kupiga kura,labda kama Tume ya Taifa ya Uchaguzi itafanya marekebisho ya sheria hii”alisema Mpanduji.
Alisema teknolojia hii BVR haitatumika katika kupiga kura bali itatumika tu katika kujiandikisha.
 
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Hamid Mahamoud Hamid alisema uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapiga kura umeshafanyika  na kwa sasa uandikishaji utafanyika katika vituo vilivyo katika ngazi ya vitongoji ,vijiji na mitaa.
 
“Kwa utaratibu huu wa sasa vituo vya kujiandikishia vimeongezeka kutoka 24,919 hadi kufikia 40,015 ambavyo vimewekwa katika ngazi za vitongoji ,vijiji na mitaa ili kuwzesha kuwa karibu zaidi na wananchina hivyo kupunguza  malalamiko ya umbali wa vituo vya kujiandikisha na kuongeza mwamko wa kujiandikisha na kupiga kura”alisema Hamid.
 
Aidha alisema kuwa Tume imejiandaa vyema katika mchakato huo ili kuhakikisha kuwa shughuli zote zilizopangwa kwenye ratiba zinafanyika kwa muda uliopangwa ikiwa ni pamoja na kufikisha vifaa vya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika maeneo husika kwa muda uliopangwa.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>