Mabasi yakiwa yamepaki katika kituo kipya cha mabasi Nanenane
Hili eneo ambalo kuna Manyasi ni eneo ambalo limetengwa maalum kwa ajili ya kuweka sehemu ya abiria kungojea usafiri au walio na wageni kungojea watu wao lakini hakuna kilicho jengwa , hali inayosababisha usumbufu mkubwa.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Baadhi ya Abiria na watu wanaongoja ndugu zao wakiwa wamekaa katika manyasi huku wakiwa hawana eneo maalum la wao kukaa, jambo ambalo linasababisha wapigwe na jua pia Mvua ikinyesha hakuna pa kujihifadhi.
Madereva na makonda wakiwa katika eneo hilo jipya la kituo cha basi
Abiria wakiwa wamekaa tuu bila mpangilio
Biashara zinaendelea
Swali linakuja hapa kwa Halmashauri ya Jiji, Je wakati kituo hiki cha basi kinazinduliwa hamkuona kuwa kunatakiwa kuwe na sehemu ya mapumziko? Wananchi wanaomba muwawekee eneo la mapumziko kulipo kuendelea kukaa katika majani ambayo hata hivyo yatakuwa mavumbi siku chache zijazo
Picha na Mbeya yetu