Ndugu, Yaya na Kolo Toure wamepewa taarifa za kifo cha mdogo wao Toure Oyala Ibrahim wakati timu yao ya Ivory Coast ikiendelea na kombe la dunia nchini Brazil.
Mdogo wa wachezaji hao wa Manchester City na Liverpool amefariki jana akiwa na umri wa miaka 28 jijini Manchester kwa saratani ikiwa ni saa mbili baada ya Ivory Coast kufungwa mabao 2-1 na Colombia.
Mdogo wa wachezaji hao wa Manchester City na Liverpool amefariki jana akiwa na umri wa miaka 28 jijini Manchester kwa saratani ikiwa ni saa mbili baada ya Ivory Coast kufungwa mabao 2-1 na Colombia.
Chama cha soka cha Ivory Coast kimetoa pole kwa Yaya na Kolo imewataka wananchi kuwakumbuka katika sala wakati huu mgumu kwao.