Uchunguzi umeanza asubuhi hii kujua chanzo cha kuzuka kwa moto karibu na hostel za wasichana katika skuli ya sanaa na lugha (School of Humanities) katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) usiku wa kuamkia leo. Athari za moto huo bado hazijajulikana.
Wakaazi wa mji huo walisikia vingo'ra vya magari ya zimamoto yakielekea chuoni huko kwa kasi, na miali mikubwa ya moto kuonekana katika vilima vya Chimwaga kipo chuo hicho usiku wa manane. Taarifa zaidi tutapeana kadiri zitavyotufikia