Mkali wa muziki wa rege nchini, Innocent Nyanyagwa na bendi yake wakitumbuiza kwenye tamasha la 17 la ZIFF 2014 linaloendelea kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Innocent Nyanyagwa na Back Vocalist wake wakishambulia kwenye tamasha la 17 la ZIFF 2014 ndani ukumbi wa Mambo Club-Ngome Kongwe.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Ras Inno akiwapa mzuka mashabiki wake kwa kuruka na wamasai ndani ya Ngome Kongwe alipotoa show ya aina yake baada ya kuhudhuria tamasha la ZIFF miaka nane iliyopita.
Watu weweeee....Haire rastafarai.....full mzuka babaake.!
Kuna watu wamebarikiwa na nywele zao, hata mikia ya Pweza haioni ndani...mmoja wa mashabiki wa muziki wa reggae aliyenivutia na nywele zake zinazoonekana kutunzwa... hapo kazizungusha je akiachia mpaka magotini hizo.
Baadhi ya raia wa kigeni waliofurika kwenye ukumbi wa Mambo Club ndani ya Ngome Kongwe wakichizika na burudani yake rege kutoka kwa Ras Inno (hayupo pichani).
Mmoja wa raia wa kigeni akichukua matukio mbalimbali wakati Ras Inno akitoa burudani ndani ya tamasha la 17 la ZIFF.
Mwenyekiti wa Wananchi Group, ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la 17 la ZIFF 2014, Richard Alden (wa pili kulia) akiwa na Mtaalamu wa masuala ya habari ZIFF, Bw. Dave Ojay ( wa pili kushoto) walipokuwa wakishuhudia Ras Inno alipokuwa akitoa burudani na bendi yake.
Katika kuongeza ladha kwenye burudani yake Ras Inno aliita couples mbili jukwaani kwa ajili ya kuimba na kucheza naye.
Couples hao hawakusita na walijivinjari kwenye jukwaa la tamasha la ZIFF 2014.
Ras Innocent akiwatambulisha Couples hao.
Yes i love Tanzania.....Mwanadada wa kizungu akiipa fagio nchi ya Tanzania na kwamba watu wake ni wakarimu sana....Mungu atupe nini jamani..? Gunia la chawa ama...? Tudumishe Upendo na Amani baina yetu.
Marissa Himid Yusuph akiteta jambo na MC wa tamasha la ZIFF 2014, Muslim Nassor.
Oooh give me a hug lil' bro...you are the best......!!!
Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala akipata Ukodak na mdau huku Ras Inno akiendelea kutoa burudani.
MC's wa tamasha la 17 la ZIFF 2014, Muslim Nassor (kulia) na mwanadada mrembo Vanessa wakishuhudia burudani kutoka kwa mkali wa reggae nchini Innocent Nyanyagwa (hayupo pichani).
Muslim Nassor na mdau kwenye tamasha la 17 la ZIFF 2014 ndani ya Ngome Kongwe.
Mjasiriamali Winiefrida Nkwera watoaji huduma za vinywaji vya aina mbalimbali akitafakari jambo ndani ya ukumbi wa Mambo Club -Ngome Kongwe linakoendelea tamasha la ZIFF 2014.
Meneja wa Tamasha la ZIFF, Daniel Nyalusi “Dean” (kushoto) akisikilizwa kuhudumiwa kinywaji baada ya kazi nzito ya kuhakikisha kila kitu kimeenda sawa kwenye tamasha la ZIFF 2014. Kushoto ni msanii Bongo Movie, Irene Sanga.
Wadau wakijipatia vinywaji ndani ya tamasha la ZIFF 2014 kwenye banda la mjasiriamali Lucy Charles.
Mtaalam wa Cocktail Edwin Fanuel (kushoto) akinywa COCKTAIL inayoitwa "Blue ZIFF" huku akipozi na Joyce Joseph ndani ya tamasha la ZIFF 2014. Ukifika hapo usikose kuonja COCKTAIL hiyo.
Na. Mwandishi wetu, Zanzibar
MKALI wa muziki wa rege nchini Innocent Nganyagwa anajiandaa kutoa filamu inayohusu maisha yake kama sehemu ya kufunza kizazi kijacho kuhusu muziki huo.
Filamu hiyo ambayo itabeba maisha yake ya kuishi katika muziki wa rege inatolewa kama ile ya Jimmy Clief The hader they Come.
Nganyagwa mwenye albamu nne na tuzo tano za hapa nyumbani alisema pamoja na kukaa kimya kwa muda mrefu alikuwa hajaondoka katika muziki wa rege lakini alikuwa anafundisha vijana ili rege iwe na undelevu nchini.
Nganyagwa ambaye alitumbuiza kwenye viunga vya Mambo Club iliyopo Ngome Kongwe amesema kwamba amekuja katika tamasha la ZIFF akiwa na mpya nyingi kuonesha wazi kwamba hakuwa mkaa bure.
Akijibu swali kuhusu mahadhi ya muziki wake na imani yake ya kirastafarian amesema kwamba muziki wa rege japo upo ndani ya imani ya kirasta, unasimama wenyewe ndio maana mtu kama yeye hapigi rege ya Jamaica kama ilivyokuwa kwa Jimmy Clief, Burning Spear au Bob Marley.
Amesema muziki wake ni wa kitanzania kwa sababu taifa hili lina vionjo vingi vya kufanya katika kuuza utamaduni wake nje kupitia muziki.
Amesema japo miondoko ya mfumo wa Babylon bado ipo kuna mstari mwembamba sana kati ya dini ya rasta na muziki wa rege na mwitikio wa muziki wa ukombozi.Hata hivyo amesema kwamba sasa hivi anapiga muziki ‘mtamu’ (sweetie reggae) muziki wa mapenzi.
Akizungumza uuzaji wa muziki wa Tanzania nje, amesema ipo haja ya wasanii kuacha kukopi na kupest (kunakiri) kwani kwa kufanya hivyo hawauzi utamaduni na hivyo wanainyima nchi fursa ya kujulikana mwisho.
“Ipo haja ya kutangaza utamaduni wetu” alisema Nganyagwa.
Aidha aliitaka serikali kuwekeza katika muziki kwa kuingilia usambazaji wa bidhaa hizo ili wasanii waweze kunufaika zaidi kuliko sasa.