Kuna lori lililokuwa limebeba kontena limejaribu kupita daraja linalounganisha Ukonga
(Banana)- Tabata Segerea- Kinyerezi na Mbezi limeharibika kabisa kwa kutumbukia na lori , kwa sasa foleni ni kubwa magari yote yanarudi, kwa wanaotoka mjini ni vyema kutumia njia ya Vingunguti kupitia Barakuda kwenda Segerea, Kinyerezi na Mbezi kwani daraja limearibika sana.
NI VYEMA SHERIA IKACHUKUA MKONDO WAKE, haiingi akilini mjinga mmoja kukata mawasilino wa watu wote kwenye njia muhimu kama hii.Mfumo wa kudhibiti malori ya mizigo ni dhaifu sana nchini, madereva wangepewa route za kupita pale wanapotoa mizigo bandari na wanapoingiza mizigo hapa mjini kutoka mikoani wahusika mmeliona hili mpaka linatokea yametokea mangapi. Daraja hili mwisho ni tani 10 kuna vibao vimeandikwa kabisa lakini kunafanyika mambo kama haya.