Serikali ya Uganda Jumatano wiki hii imeipiga marufuku moja ya TV za nchi hiyo kutokucover matukio yoyote ya Rais baada ya kuonesha kwenye TV picha za Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni akiwa ‘amesinzia’ bungeni.Kwa mujibu wa AFP, msemaji wa serikali Ofwono Opondo, amethibitisha kuwa kituo cha NTV Uganda kimezuiwa kucover matukio ya Rais kutokana na tukio hilo.
“We have suspended their coverage of the president as we reconsider our relationship with them,”, alisema Opondo.Hata hivyo Opondo amesema kituo hicho hakijasimamishwa moja kwa moja kucover matukio ya Rais, bali itakuwa ni kwa muda.“The suspension should not be permanent, it’s temporary, to make them think.”
Kituo NTV Uganda kimesema kuwa bado hakijapata taarifa za kufungiwa kucover matukio ya Rais.
Source: Standard Digital