Timu ya taifa ya Uholanzi imekuwa timu ya kwanza kufuzu mkondo wa pili wa kombe la dunia baada ya kuishinda Australia mabao 3-2 katika mchuano wa kusisimua wa kombe la dunia huko Rio de Janeiro, siku ya Jumatano.
Uholanzi, iliiadhibu kwa urahisi Uhispania mabao 5-1 katika mchuano wao wa kwanza, lakini walilazimishwa kujikaza katika mchuano huu wa pili ilikupata ushindi. Arjen Robben aliweka Uholanzi kifua mbele katika dakika ya 20.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Dakika moja baadaye, Australia walisawazisha kupitia mchezaji Tim Cahill. Mile Jedinak aliifungia Australia bao la pili kupitia penalti katika dakika ya 58 baada ya Daryl Janmaat kuugusa mpira ndani ya eneo lao la lango.
Uholanzi ni timu ya kwanza kufuzu kwa mkondo wa pili wa kombe la dunia.Kuendelea kwa Uholanzi katika raundi ya pili ya kombe la dunia, bado kutaamulia katika mchuano wa mwisho kwani tofauti ya mabao yaweza kutatanisha.
Katika hatua nyingine timu ya taifa ya Hispania wameweka rekodi ya kuwa bingwa mtetezi wa kwanza kutolewa kwa kufungwa mechi mfululizo.