Michuano ya kombe la dunia imezidi kushika kasi kwa michezo itatu iliyopigwa usiku wa kuamkia leo. Mchezo wa kwanza ulikuwa kati ya wawakilishi wa Afrika Cameroon dhidi ya Mexico, na wamexico wakaondoka na ushindi wa goli moja kwa bila.
Mechi ya pili iliyomalizika kwa kushuhudia mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia Spain wakidhalilishwa kwa kipigo kizito kutoka kwa Uholanzi.Spain walianza kuliona lango la Uholanzi kwa mkwaju wa penati wa Xabi Alonso, lakini Robin van Persie akaisawazishia Uholanzi kabla ya mapumziko.
Kipindi cha pili Uholanzi walirudi kwa kasi na kufanikiwa kuongeza magoli mengine manne kupitia Van Persie, Robben aliyefunga mawili na beki Stephan de Virj akaongeza la tano. Mpira ukamalizika kwa Spain kufungwa 5-1. Mchezo wa mwisho ulikuwa ni kati ya Chile vs Australia, ambapo Australia ilikubali kichapo cha mabao matatu kwa moja(3-1)