Mama Mzazi wa Kijina Mwanaidi Bi Jina akimpatia uji mtoto wake wakiwa katika wodi ya hospitali ya mnazi mmoja wakiendelea na Tiba baada ya kuhamishiwa hapo kutoka hospitali ya jeshi bububu, ili kuendelea na huduma hiyo ya matibabu wakisubiri kupata michango ili kuweza kumsafirisha nje ya nchi kupata matibabu zaidi.
Shukrani kwa Wananchi waliojaliwa kutowa msaada kwa Ndg Mwanaidi ili kupata fedha za kumuwezesha kusafirishwa nje ya Nchi kupata utibabu wa jaraha lake la kuunguwa na moto.
Natangulia shukrani kwa Wananchi waliotoa msaada wao kumchangia Kijana Mwanaid Saleh kupitia Mtandao wa Tigi Pesa kupitia Na. 0715 424152 - Othman Maulid, Mchango wao unafika na kuhifadhia Benki ya Watu wa Zanzibar ( PBZ) Tawi la Malindi Zanzibar katika AC N0 051206007686. yenye Jina la PAVU OMAR AMEIR.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Shukrani kwa Wananchi waliotuma Pesa Tigo Pesa.
Kupitia Wakala wa Tigo Pesa Shs. 10,000/= , Ndg. Omar Shamte Haji Shs.4000/-, Ndg. Ziada Kikunga Shs.6000/- Khamis Suleiman kupitia M-Pesa Shs.48,000/- na Maryam Hilal Shs.3000/-
Natoa shukrani kwao na Inshala Mwenyezi Mungu akiwajalia kila la kheri na mafanikio katika shughuli zao za kila siku kwa baraza za Mola Subuhana Wataal.
Kwa sasa Namshukuru Mwenyezi Mungu kiasi cha Fedha kilichopatikana na kuwekwa katika Akaunti hiyo ni Shs 444,000/- Mpaka leo 13-6-2014.