Mtoto aliyekutwa amefariki baada ya kutupwa eneo la Kawe-Beach na kufungwa plasta mdomoni na puani.
Katika hali isiyo ya kawaida mwanamke mmoja ambaye hakujulikana jina lake wala kujua anapoishi, anasadikika kutenda ukatili na unyama wa hali juu kwa kumuua mwanaye na kisha kumtupa pembezoni mwa barabara ya kwenda Kawe-Beach.
Moja wa wasamalia wema akimfunika mtoto huyo.
Wavuvi wa eneo hilo waliona mfuko pembezoni ukiwa na damu hali ambayo iliwashtua na kuamua kusogea karibu ndipo walipomkuta mtoto huyo mwenye jinsi ya kike akiwa amefariki huku akiwa amefungwa plasta mdomoni na puani.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wakazi wa eneo la Kawe na wapita njia wakiangalia kichanga hicho baada ya kuokotwa na wavuvi.