Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

NUSU MWAKA UMEFIKA, JE MALENGO YAKO YAMEFIKIA WAPI?

$
0
0
Ungwe ya kwanza ya mwaka 2014 inamalizikia, naamini ulikuwa na vitu ambavyo ulidhamiria kuvifanya mwaka huu. Sasa ni wakati wa kujaribu kupitia je mambo yako au mipango yako imefikia wapi na je unaendelea vizuri au vibaya? Ni vizuri kufuatilia mambo yako yanavyokwenda wakati nusu ya kwanza inaenda kuisha na tunatarajia kuingia nusu ya pili hivi karibuni.
Unapoangalia nyuma ulikotoka kitu cha kujichunguza ni mafanikio gani uliyopata miezi mitano inayoishia na hasara gani au vikwazo ulivyokutana navyo na unajirekebishaje unapokwenda nusu ya mwisho kwenye mwaka 2014?

Uchumi wako unakwendaje?
Je mwenendo wa fedha zako unakwendaje katika nusu hii ya kwanza? Matumizi yako na mapato yanaendana? Je umetengeneza madeni mengi au umeweza kuweka akiba kwa ajili ya baadaye? Kama ulipanga kuanzisha mradi hebu angalia kama mradi umeanza na kama haujaanza ujiulize tatizo ni nini?

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Je kwenye mahusiano yako yanakwendaje?
Ni vizuri kujua mahusiano yako yanaendeleaje na kama yana mwelekeo unaostahili.Kam umekuwa unazunguka na watu sahihi inawezekana mahusiano yako yakawa yenye tija ila kama umekuwa na watu ambao sio sahihi hujachelewa kujiondoa na kujitenga nao. Kumbuka maisha yako ya baadaye yanakuhitaji ufanye maamuzi sahihi ili usipate majuto baadaye.

Taaluma yako je?
Hebu fuatilia kitaaluma unaendeleaje na umeweza kufanikisha kitu gani katika kipindi hiki. Je kuna kitu ulipaswa kufanya na hakijafanyika? Kama ulipanga kujiendeleza je umeweza kuchukua hatua yeyote?

Imani yako ikoje?
Mara nyingi watu wengi huiweka mbali imani wakifikiri ni ushamba au ujinga ingawa wanaiihitaji. Unaweza kusema huna imani lakini kuna kitu unakiamini ambacho kinaweza kuwa ni sahihi au sio sahihi. Lazima ujue kwa miezi hii sita inayoishia ukoje kiimani? Hata kama una biashara vile vile ujue namna biashara yako inavyokwenda, je inakuwa au inashuka? Ongeza ubunifu na weledi katika kila unachokifanya.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>