Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

CHRIS BROWN AKIRI KUVUNJA SHERIA, AONGEZEWA KIFUNGO CHA SIKU 131 JELA

$
0
0
 Ijumaa (May 9), Chris Brown alifikishwa katika mahakama ya Los Angeles ambapo alikiri kuvunja sheria/ masharti ya probation yake baada ya kumshambulia mtu mwaka jana huko Washington, D.C.
Jaji anaeisikiliza kesi yake, James R. Brandlin alimhukumu mwimbaji huyo kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa hilo, lakini alitoa siku 234 alizozitumikia tayari akiwa rehab na jela kwa hiyo anatakiwa kumalizia siku 131 zilizobaki akiwa jela.
Breezy alikuwa anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka minne jela lakini Jaji alimpunguzia kwa kuifikiria hali yake ya afya kwa kuwa anasumbuliwa na ugonjwa unaomsababishia hasira kali.
Jaji amempa amri pia ya kuhudhuria matibabu mara mbili kwa wiki na kupima vipimo vya dawa za kulevya mara tatu kwa week bila kuchagua siku.
Mbali na kifungo hicho, Chris Brown bado anakabiliwa na kesi ya kumshambulia mtu kwa kumpiga ngumi na kesi hiyo imepangwa kusikilizwa June 25.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>