Askari polisi wakiwalinda mahabusu wawili kati ya sita wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, wakiwa wameng'ang'ania mlingoti wa Bendera ya Taifa huku mnoja akiwa mtupu mara baada ya kutoroka toka kwenye msafara wa mahabusu waliokuwa wakiingia mahakama ya wilaya ya Nyamagana na kisha mmoja wao kuvua nguo.
Inspector Henry akiwasihi mahabusu hao wawili wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, kuachia mlingoti wa Bendera ya Taifa na kurudi kwenye chumba cha mahakama kwaajiri ya taratibu za kesi.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Inspector Henry (shati la bahari) akiwa na Inspector Veda (mwenye koti) wakisikiliza hoja za Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu akiwa ameng'ang'ania mlingoti wa Bendera ya Taifa uliopo katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza, ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji Na. 32/2012.
Inspector Veda (mwenye koti) akichukuwa maelezo ya Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu akiwa ameng'ang'ania mlingoti wa Bendera ya Taifa uliopo katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza, ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji Na. 32/2012. akiwa na mwenzake Hamis Ramadani (30).
Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari mahabusu hao walikubali kurejea chumba cha Mahakama.
Nje ya Mahakama kuelekea lango kuu.
Wananchi wamefurika viwanja vya mahakama.
Mashuhuda.