Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

BING YAMTAJA BEYONCE KAMA MTU ALIYETAFUTWA ZAIDI KWENYE MTANDAO MAREKANI MWAKA 2013, OBAMA AFUNGA LIST, BIEBER AFUNIKA UINGEREZA

$
0
0


Tukiwa tunaelekea kuumaliza mwaka 2013 vyombo mbalimbali vimeendelea kutoa tathmini ya mwaka kwa kazi wanayoifanya na kutoa picha ya kile kilichopendwa zaidi na watu.
Search engine ya Bing imetoa majina kumi ya watu waliotafutwa zaidi kwenye mtandao huko Marekani na Beyonce Knowles ameshika nafasi ya kwanza.
Beyonce amemfunika Kim Kardashian ambaye ameshika nafasi ya pili na Rihanna aliyeshika nafasi ya tatu.
Rais wa Marekani Barack Obama amefunga list ya majina kumi, na kushika nafasi ya kumi huku wanamuziki wakionekana kuiteka list hiyo.
Beyonce pia ameshika nafasi ya kwanza kwa wanamuziki waliotafutwa zaidi mwaka huu kupitia mtandao kwa mujibu wa Bing.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Hata hivyo Justin Bieber ameonekana kung’aa zaidi Uingereza ambapo ameshika nafasi ya kwanza kama mtu aliyetafutwa zaidi Uingereza akifuatiwa na Queen Bay, huku akishika nafasi ya sita kwa upande wa Marekani.
Hii ni orodha kamili ya watu waliotafutwa zaidi Marekani na Uingereza kwa mujibu wa Bing.
The most-searched people in the U.S.:
1.            Beyonce Knowles
2.            Kim Kardashian
3.            Rihanna
4.            Taylor Swift
5.            Madonna
6.            Justin Bieber
7.            Nicki Minaj
8.            Amanda Bynes
9.            Miley Cyrus
10.          Barack Obama
The most-searched people in the U.K.:
1.            Justin Bieber
2.            Beyonce Knowles
3.            Kate Middleton
4.            Selena Gomez
5.            Nicole Scherzinger
6.            Rihanna
7.            Kim Kardashian
8.            Taylor Swift
9.            Emma Watson
10.          Kelly Brook

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>