Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

BALOZI LIBERATA MULAMULA NA MUMEWE WAWASILI COLUMBUS, OHIO

$
0
0

 Baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio wakijiandaa kuelekea uwanja wa ndege wa Columbus, Ohio kumpokea Mhe. Liberata Mulala atakaye kuwa mgeni rasmi kwenye fundraising Dinner itakayofanyika leo Jumamosi April 19, 2014 na muziki kupigwa na Dj Luke kutoka DC ambaye tayari ameishatia timu na kusema pamoja na fundraising amekuja kuwapa mashabiki wake wa Ohio zawadi wa Pasaka. Fundraising itafanyikia Comfort Inn 1213 E. Dublin Granville Road, Columbus, OH, 43229 na kiingilio ni $15. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio Bwn. Jimmy James, Mjumbe Eliud Mashambo, Katibu Bi. Happiness Salukele na Deo Mwalujwa ambaye ni mmiliki wa Black Diamond Tours aliyetoa usafiri wa kumchukua Mhe. Balozi kutoka uwanja wa ndege mpaka hoteli aliyofikia.
 Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio wakimpokea Mhe. Balozi Liberata Mulamula (wapili toka kulia) wengine katika picha toka kushoto ni Mjumbe Eliud Mashambo, Mume wa Balozi Bwn. George Mulamula, Deo Mwalujwa, Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio Bi. Happiness Salukele na Joe Ngwilizi ambaye ni Mjumbe.


 ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea shada la maua kutoka kwa mtoto Luluwa Rashid mara tu baada ya kuwasili Hotel ya Hilton alikofikia.
 Picha ya pamoja kutoka kushoto ni mweka hazina wa Jumuiya Bi. Vera Teri, Mhe. Liberata Mulamula, Mtt. Luluwa Rashid, Mjumbe Bwn. Joe Ngwilizi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio Bwn. Jimmy James.
 Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio wakifanya kikao cha maandalizi ya mwisho mwisho ya Fundraising Dinner itakayofanyika leo Jumamosi April 19, 2014 katika ukumbi wa Comfort Inn.
 Kutoka kushoto ni Mume wa Balozi Bwn. George Mulamula, Balozi wa heshima Bwn. Patrick Griswold na Mhe. Balozi Liberata Mulamula wakifanya mazungumuzo ya pamoja na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania wa Columbus, Ohio ndani ya mgahawa wa Hilton hotel ya mjini Columbus, Ohio.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio Bwn. Jimmy James na Katibu Bi. Happiness Salukele wakifuatilia mazungumuzo ya Mhe. Balozi Liberata Mulamula (hayupo pichani) alipofanya mazungumuzo na uongozi wa Jumuiya na Balozi wa Heshima Bwn. Parick Griswold.
 Mazungumuzo ya Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Heshima Bwn. Patrick Griswold pamoja na Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio yakiendelea.
 Picha ya pamoja kutoka kushoto ni Alexas Griswold (mtoto wa Balozi wa Heshima), Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio Bwn. Jimmy James, Balozi wa Heshima Bwn. Patrick Griswold, Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio Bi. Happiness Salukele, mjumbe Joe Ngwilizi, Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Mtt. Luluwa Rashid, Mume wa Balozi Bwn. George Mulamula, mweka hazina wa Jumuiya Bi. Vera Teri na mjumbe bwn. Eliud Mashambo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>