Waombolezaji wakiwa msibani Jana kushoto mwenye tisheti nyeusi ni Mratibu wa Skylight Band.
Mpiga Gita mahiri wa bendi ya Skylight Chill challa amezikwa jana kwenye makaburi ya Mwananyamala kwa kopa na mamia ya watu na wanamuziki wenzie.Marehemu Chill challa alifariki Tar 17-04-2014 hospitali ya Taifa ya Muhimbili.Chanzo cha kifo cha marehemu ni shinikizo la damu ambapo kabla ya kifo chake alikuwa katika afya njema,lakini Usiku wa Tar 16 marehemu alidondoka gafla bafuni na ndipo alipkimbizwa hospitalini.
William Malecela akijadili jambo na Mkurugenzi wa Skylight band ili kuweka mambo sawa kabla ya Mwili wa marehemu kuwasili.
Madaktari walijitaidi kwa kila hali na mali kuokoa uhai wa marehemu lakini ilishindikana kutokana na shinikzo la damu kuwa kubwa sana na ndipo Chill challa akafariki dunia,Marehemu Chill challa ameacha Mke na watoto wawili,Marehemu alikuwa ni mpiga gita mzoefu na mahiri ambaye amepitia karibu bendi zote kubwa na kongwe nchini kama Akudo,Fm academia Nk.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Baadhi ya waombolezaji wakibadilishana mawazo Katikati ni Mwanamuziki wa Skylight band Joniko Flower
Waombolezaji wakiendelea kubadilishana mawazo wakati wakisubili mwili wa marehemu Kufika,Mwenye Baibui nyeusi ni mke wa Chicago Matelephone na wanamuziki wa Skylight band
Mkurugenzi wa Skylight Band akijadili jambo na Aneth Kushaba ili kuweka mambo sawa kabla ya Mwili wa marehemu kuwasili.
Gari iliyobeba Mwili wa marehemu Chill Challa likiwasili Nyumbani kwa marehemu
Ndugu na Jamaa wakishusha Mwili wa marehemu Chili Challa
Mwili wa Marehemu ukishushwa kwa ajili ya ibada
Mchungaji wa kanisa alipokuwa Anasali marehemu akiongoza ibada ya kumuombea Marehemu Ayoub Songoro maaru Chill challa aliyekuwa mwanamuziki na mpiga Gita wa Skylight Band.
Misa ya kumuombea Marehemu akiendelea Nyumbani kwake Mwananyamala
Mke wa marehemu akiwa na majonzi
Meneja wa bendi Ya Skylight Aneth Kushaba akiaga mwili wa marehemu
Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu
Mkurugenzi wa Skylight Band akiaga Mwili wa marehemu
Watoto wa marehemu wakiwa na majonzi ya kuondokewa na baba yao kipenzi
Kaka wa marehemu akiaga mwili wa mdogo wake kwa huzuni kubwa
Mwili wa marehemu ukipandishwa kwenye gari Tayari kwenda kuzikwa baada ya ibada ya kumuombea
Msafara ukielekea makaburi ya Mwananyamala kwa kopa
Mwili wa marehemu ukishushwa kaburini tayari kwa kuzikwa
Wanamuziki wenzake na marehemu wakifuatilia mazishi ya mwenzao
Mchungaji akisoma neno
Mchungaji akirusha udongo kuonyesha ishara ya kuaza maziko
Mke wa marehemu akirusha udongo ndani ya kaburini
Watoto wa kiume wa marehemu wakirusha udongo kaburini kumzika baba yao
Kaka wa marehemu akiwa akimzika mdogo wake
Mkurugenzi wa Skylight Band akirusha udongo kumzika msanii wake
Aneth kushaba akirusha udongo kumzika marehemu
Waombolezaji wakiwa wanafuatilia maziko kwa huzuni kubwa
Mchungaji akiweka msalaba kwenye kaburi la marehemu
Mke wa marehemu akiweka shada la maua kwenye kaburi
Watoto wa marehemu wakiweka shada la maua kwenye kaburi na Baba yao
Ndugu wa Marehemu wakiweka Shada la maua
uongozi mzima wa Skylight band unawashukuru wale wote waliojitoa kwenye msiba huu na Mungu awabariki.