Asha Manga ,25, mkazi wa Tarafa ya Turiani Wilaya ya Mvomero mjini, anaumwa sana kwani anasumbuliwa na uvimbe kwenye taya unaoendelea kukua kila siku. Asha anayeishi na mama yake, Halima Juma baada ya baba yake mzazi, Juma Manga kufariki dunia, amekuwa akitumia muda mwingi kulia na kusema anakufa huku anajiona kufuatia kukosa kiasi cha shilingi milioni nne za matibabu.
Akizungumza Ijumaa, Asha alisema: “Nikiwa kidato cha nne ndipo hili tatizo liliponianza, nilihisi ni jipu lakini kadiri siku zilivyosogea, uvimbe uliongezeka.
“Nilikwenda Hospitali ya Wilaya ya Turiani nikafanyiwa uchunguzi na kupewa dawa, nikapata nafuu na kuendelea na masomo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
“Mwaka 2008 hali ilinirudia tena nikashindwa kuendelea na masomo yangu ya kidato cha tano. Nilikwenda hospitali ambapo daktari alinichunguza na kunipatia dawa lakini sikupata nafuu.
“Nilirudi pale hospitalini ambapo daktari aliniambia natakiwa kufanyiwa matibabu ya haraka kwani naweza kupata tatizo la saratani.
“Nilipoambiwa hivyo, nililia sana kwani nilijua mwisho wa maisha yangu umefika kwa sababu mimi na mama yangu ni maskini, maisha yetu magumu… hata kula yetu ni ya shida.”
Asha anaeleza kuwa, baada ya kuambiwa hivyo alifikishwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa msaada wa Mkurugenzi wa Asasi ya Wezesha ya Morogoro, Lusako Mwakiluma, ikabainika taya lake limeharibika na zinatakiwa shilingi milioni 4 ili awekewe lingine. Msomaji wetu, Asha anahitaji msaada wako ili apone hivyo unaweza kuchangia chochote kupita namba 0713 33 74 49, 0767 44 81 86 au akaunti namba 01 52 39 29 51 2000 ya CRDB.