NOOR SHIJA
Kwa miaka mingi, watu wenye ulemavu wa kuona, wasioona kabisa na wale wenye uono hafifu, wengi wao wamekuwa wakitumia fimbo maalumu (white cane) kwa ajili ya kutambua vitu vilivyo mbele yao.
Hata hivyo, mwanasayansi Dk Stephen Hicks wa Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza, amegundua teknolojia mpya ya miwani inayowawezesha watu wenye ulemavu wa kuona kutambua vitu vilivyo mbele yao, maandishi kwenye mabango na majina ya mitaa kupitia miwani maalumu iliyopewa jina la ‘Smart Glasses.’
Kwa mujibu wa Dk Hicks, teknolojia hiyo mpya inafuatia teknolojia nyingine ya miwani, ambayo humwezesha mtu mwenye ulemavu wa kuona, kupata picha ya vivuli ya vitu vilivyo jirani naye, ikiwemo binadamu.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Hata hivyo, Dk Hicks amekuja na uvumbuzi mwingine wa ‘Smart Glasses’ inayomsaidia mtumiaji kujiongoza mwenyewe katika maeneo ambayo hayafahamu kwa kusoma vibao vya maelekezo, kama vile majina ya mitaa na vituo vya basi.
Dk Hicks anasema kuwa miwani hiyo inamfanya mtu mwenye ulemavu wa kuona kuweza kujitegemea kwa kiwango kikubwa, ikiwemo kufahamu maneno yaliyoandikwa kwenye mabango ya matangazo, mitaa na orodha ya vyakula hotelini.
Kwa mujibu wa teknolojia hiyo ya Dk Hicks, miwani hiyo imetengenezwa kwa kuwekwa kamera ambazo zinarekodi picha, yakiwemo maandishi na kuyatambulisha kwa sauti kwa mtumiaji. Mfano, orodha ya vyakula hoteli, miwani hiyo inarekodi maneno na kuyatamka kwa sauti kwa mtumiaji.
Dk Hicks anasema kuwa miwani hiyo itasaidia maelfu ya watu wenye ulemavu wa kuona kuweza kumudu kufanya shughuli zao bila utegemezi wa watu wengine, ikiwemo kufahamu maelekezo yanayotokana na mabango ya barabarani, hasa majina ya mitaa na vituo vya mabasi.
Zaidi ya miaka mitatu, Dk Hicks amekuwa akitengeneza miwani hiyo ali yoweka kamera na programu inayomsaidia mtumiaji kubaini kitu na miwani hiyo inamtamkia kwa maneno.
Ulemavu wa macho ni hali ya kukosa kuona kutokana sababu zinazohusiana na mishipa, kuna viwango mbalimbali vimetengenezwa ili kuelezea kiwango cha kukosa kuona, ambapo upofu kamili ni ukosefu kamili wa kuona maumbo na mwanga na hurekodi kliniki kama NLP, kifupishi cha “No Light Perception” au kukosa kuona mwanga.
Hata hivyo, kwa mujibu wa wataalamu wa macho, watu wenye ulemavu huo ambao macho yao bado hayajaharibika, wanaweza kutambua kukiwa na mwanga ingawa hawaoni kwa ukamilifu. Ishara za mwanga za lengo hili husafiri kupitia njia ya ‘retinohaipothalamia,’ kwa hivyo mishipa ya jicho iliyoharibika kupita mahali ambapo njia ya ‘retinohaipothalamia’ hutokea kwenye jicho siyo kizuizi.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), zinaeleza kuwa visababishi vya upofu wa kawaida duniani kote katika mwaka 2002 vilikuwa mtoto wa jicho asilimia 47.9, glakoma asilimia 12.3, kuzorota kwa seli kunakohusiana na umri asilimia 8.7, konea kutopitisha nuru asilimia 5.1 na kuharibika kwa retina kunakosababishwa na ugonjwa wa kisukari asilimia 4.8, pia upofu tangu utotoni asilimia 3.9, trakoma asilimia 3.6 na onkoseresiasisi asilimia (0.8).
Kulingana na suala la maambukizi ya upofu duniani, idadi kubwa ya watu katika nchi zinazoendelea na uwezekano mkuu wao kuathiriwa unamaanisha kuwa visababishi vya upofu katika maeneo hayo ni muhimu zaidi kiidadi.
Mtoto wa jicho husababisha zaidi ya kesi 22,000,000 za upofu na glakoma kesi 6,000,000, wakati ukoma na onkoseresiasisi husabaisha kupofuka kwa takriban watu 1,000,000 duniani kote.
Idadi ya watu, wanaokuwa vipofu kutokana na trakoma imeshuka kwa kasi katika kipindi cha miaka 10 kutoka milioni sita hadi milioni 1.3, hivyo basi kuiweka katika nafasi ya saba kwenye orodha ya visababishi vya upofu duniani kote.
Xerophthalmia (ukavu wa macho), inakadiriwa kuathiri watoto milioni tano kila mwaka; 500,000 hupata konea inayofanya kazi, na nusu yao huwa vipofu. Vidonda vya konea pia ni kisababishi kikubwa cha upofu wa jicho moja duniani kote na uhusishwa na kesi zinazokadiriwa 850,000 za upofu wa konea kila mwaka katika eneo la nchi ya India peke yake. Kutokana na hayo, kuharibika kwa konea kutokana na sababu zote sasa ndiyo sababu ya nne kuu ya upofu kimataifa (Vaughan & Asbury’s General Ophthalmology).
Watu katika nchi zinazoendelea wanaweza kuathiriwa zaidi na upofu kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuiwa au kutibiwa wakilinganishwa na wenzao katika mataifa yaliyoendelea.
Ingawa kuharibika kwa macho huwaathiri sana watu waliozidisha miaka 60 katika maeneo yote, watoto walio katika jamii maskini wanaweza kuathiriwa sana na magonjwa yanayosababisha upofu wakilinganishwa na wenzao kutoka jamii tajiri.
MWANANCHI