Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi alipowasili katika viwanja vya CCM Kisiwandui leo katika hitma na dua ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,wakati wa hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo mchana,(Picha na Ramadha Othman,Ikulu.)
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mke wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume akitia ubani wakati wa hitma ya kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,wengine pia ni wake wa Viongozi.
Miongoni mwa wake wa Viongozi wa Zanzibar walioshiriki katika hitma ya kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,akiwemo Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mama Salma Salmin (kushoto).
Mabalozi wadogo wa Nchi mbali mbali wanaofanyia kazi Zanzibar walijumuika na viongozi na wananchi katika hitma ya kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
Wajukuu wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,(wa kwanza na watatu kushoto) wakiwa katika hitma ya kumuombea dua Rais wa kwanza iliyosomwa leo katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
Viongozi na wananchi wa Zanzibar waliohudhuria katika hitma ya kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,iliyosomwa leo katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein wakisalimiana wajukuu wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,na Viongozi wakati wa hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo mchana.
Kadhi Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Sheikh Khamis Haji akitia ubani kuongoza wakati Hitma na Dua ya kumuombea Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM kisiwandui Mjini Unguja,(kushoto) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akiungana na Viongozi,Wananchi katika kumuombe dua kwa Kisomo cha Hitma iliyosomwa leo katika Ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,wakiwemo Rais wa Tanzania Alhaj Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais mstaafu wa Tanzania Mzee Mwinyi,Rais mstaafu wa Zanzibar Dk.Amani Abeid Karume,Makamo wa Rais wa Tanzania Dk.Bilali,Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Viongozi wengine (wa pili kushoto).