Wachimbaji wakiandamana leo wilayani Nzega mkoani Tabora.
Jeshi la polisi wilayani Nzega mkoani Tabora limetumia nguvu kusambaratisha maandamano ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu yaliyolenga kupinga kufungwa kwa machimbo yao ya Mwashina yaliyo jirani na mgodi wa Resolute Tanzania Limited wilayani Nzega. Mara baada ya kukaribia katika eneo la machimbo ambako maandamano yalikuwa yanaelekea,kabla hata hawajafika eneo la machimbo,ghafla polisi waliibuka na kuanza kurusha mabomu hovyo na baadaye kumkata mbunge wa jimbo la Nzega Dkt Hamis Kigwangalla ambaye kabla ya kuanza kwa maandamano hayo alifanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nzega ndogo ili kujua mstakabali wa wachimbaji hao ambao hivi karibuni waliziuiwa kuchumba na kamishana wa madini nchini Paul Masanja kwa kile kilichotajwa kuwa wamevamia eneo hilo.
Kufuatia malalamiko ya wachimbaji hao kuondolewa bila kujali gharama waliozotumia walimwomba mbunge wao aridhie maandamano hadi katika eneo la machimbo ndipo mkutano ukavunjika na maandamano yakaanza na matokeo yake mabomu ya machozi pamoja na risasi za moto. ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI Katika na purukushani hizo polisi walifanikiwa kumkamata mbunge huyo na kumjeruhi mtu mmoja kwa risasi ya moto kwenye paji la uso ambapo waliondoka nae kwenye gari pamoja na mbunge huyo.
Katika hatua nyingine hali ilikuwa tete kwa waandishi wa habari kwani askari wa jeshi hilo waliziba njia na kuwazuia waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa vitisho mbalimbali na matumisi ingawa hali hiyo ilitulia baada ya maandamano ya wachimbaji kujitokeza.
|