Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

MKUU WA MKOA WA DODOMA DR REHEMA NCHIMBI AMEZINDUA MRADI WA MAJI KIJIJI CHA CHIDIDIMO MANISPAA YA DODOMA

$
0
0
 Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akisalimiana na wanafunzi wa shule ya msingi Chididimo waliojitokeza kumlaki alipowasili kijijini hapo kuzindua mradi wa maji kijijini hapo jana.
 Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi(kushoto) akipokea taarifa ya mradi wa maji kijiji cha Chididimo manispaa ya Dodoma kama inavyowasilishwa kwake na mhandisi Mohamed Khali ( Kulia)  kutoka idara ya maji manispaa ya Dodoma wakati wa sherehe ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika jana.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
 Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akizindua mradi wa maji kwenye kijijicha Chididimo manispaa ya Dodoma jana, wengine ni wajumbe wa chombo huru cha watumiaji maji kijijini hapo.
 Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwasha mashine ya kusukuma maji kwenye mradi wa maji kijiji cha Chididimo manispaa ya dodoma muda mfupi baada ya kuzindua mradi huo.
  Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kushoto) akizungumza na  viongozi pamoja na  wananchi wa kijiji cha Chididimo kilichopo manispaa ya Dodoma kuulinda na kuutunza mradi wa maji kijijini hapo muda mfupi mara baada ya mkuu huyo wa mkoa kuuzindua mradi huo jana.
  Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (kulia) na katibu tawala Mkoa Dodoma Ndg. Rehema Madenge wakifungua na kukinga maji kwenye mradi wa maji kijiji cha Chididimo kilichopo manispaa ya Dodoma wakati wa uzinduzi wa mradi huo mapema jana. Wanaoshuhudia ni wananchi wa kijiji cha Chididimo.
  Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi akimtwika ndoo ya maji mdala Morleni Mwaluko mmoja wa wanakijiji cha chididimo, maji hayo safi kwa  sasa yanapatikana kwa urahisi na kwa karibu  kijijini hapo baada ya kukamilika kwa  mradi wa maji wa kijiji hicho, mkuu wa MKOA dodoma amezindua mradi huo mapema jana.
 Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (aliyeshika kibuyu katikati) akiimba na kuserebuka nyimbo za asili ya kigogo pamoja na akinamama wa kijiji cha Chididimo manispaa ya Dodoma kusherehekea muda mfupi baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzindua mradi wa maji kijijini hapo jana.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>