Muigizaji mkongwe wa filamu za vichekesho nchini, Kingwendu amesema wasanii wa fani hiyo wanaongoza kwa kuwa na maisha magumu kutokana kulipwa ujira mdogo katika kazi zao.
Kingwendu amesema kuna wasanii wa vichekesho wanaumwa maradhi ya kutibika ila wanakosa hata pesa za kwenda kupata matibabu.
“Sikufichi kuna msanii mmoja wa comedy anaitwa ‘Mapembe’ sio Pembe,anaumwa sana na anazunguka huku na kule kutafuta msaada ya pesa kwaajili ya matibabu,” Kingwendu ameuambia mtandao huu.
“Sio kwamba hafanyi kazi,anafanya kazi nyingi lakini ukiambiwa hicho kipato anachopata msanii wa comedy utasikitika sana. Hakuna pesa ndugu, mpaka sasa wasanii wa comedy tumefanya mchango ili tuweze kumsaidiA kidogo. Kwahiyo sisi wasanii wa comedy tunahangaika sana na maisha yetu ni magumu sana hata naweza kudiriki kusema kuliko wasanii wote. Mimi sasa hivi nikifanya kazi ya filamu nikapeleka Steps itakaa miaka mitatu wakisema haiuziki. Sasa sisi ndio kazi yetu tufenyeje? Kwahiyo nataka Watanzania wajue tuna maisha magumu,kama kuna wadau ambao wanaweza kusimamia kazi zetu wajitokeze ili kuboresha maisha yetu,” aliongeza.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Katika hatua nyingine Kingwendu amesema kutokana na ugumu wa maisha ya wasanii wa comedy wamekuwa wakifanya matangazo kwa bei ya chini mno.
“Kuna kampuni iiifanya matangazo na mimi,sikufichi pesa ambayo walinipa ni aibu. Huwezi kataa kutokana na maisha yetu,kwanza wanaanza kulialia,pesa hakuna budget ndogo sijui kimepanda kimeshuka,mpaka mnakubaliana ni pesa ndogo sana. Kwahiyo kwanza mawakala wa matangazo wanatulalia sana. Mimi tangazo kubwa ambalo lilinilipa pesa kubwa nila(……) lilinilipa shilingi milioni 2 najua hili tangazo lilikuwa na bei kubwa zaidi, ila walibana,kwahiyo mimi naomba wajirekebishe sisi tuna umuhimu na wao pia.”
SOURCE: BONGO 5