Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma – UDOM aliyekuwa anafahamika kwa jina la Godlove Benjamin, Mwaka wa Tatu aliyekuwa anasoma shahada ya Utawala wa Biashara(BBA) Kitivo cha Sayansi ya Jamii (Social Science) amefariki dunia siku ya Ijumaa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam wakati akiwa likizo ya wiki mbili na mwili wake umesafirishwakwa ajili ya mazishi, ambapo anazikwa leo siku ya Alhamis nyumbani kwao Mogumu, Musoma mkoani Mara. Sababu ya kifo chake aliugua ghafla ugonjwa wa homa ya matumbo (Typhoid).
MUNGUILAZE ROHO YA MAREHEMU GODLOVE BENJAMIN MAHALI PEMA PEPONI
AMINA