Katika kukabiliana na ugonjwa wa Malaria, Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) inayojishughulisha na masuala ya watu wenye Ualbino yenye makao makuu yake nchini Uholanzi imetoa msaada wa vyandarua 50 kwa ajili ya watoto wenye ualbino wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Msaada huo umetolewa na mwenyekiti wa JTFE, Pieter Staadegaard siku moja tu baada ya kutembelea kituo hicho na kuelezwa kuhusu upungufu wa vyandarua katika kituo hicho ambapo sasa kina watoto 228 kati yao wenye ualbino ni 142.
Akikabidhi vyandarua hivyo leo Jumamosi May 27,2017 Staadegaard alisema vitasaidia kupiga vita ugonjwa wa malaria na kwamba miongoni mwa malengo ya taasisi hiyo ni kuongeza elimu kwa jamii kuhusu masuala ya ualbino na kuwawezesha kiuchumi watu wenye ualbino.
"Nilifikika katika kituo hiki jana May 26,2017 kisha kutoa msaada wa vifaa vya michezo kwa watoto ikiwemo midoli,miwani ya kuzuia mionzi ya jua lakini pia viatu,nilipomaliza kugawa zawadi hizo viongozi wa kituo hiki wakaniambia pia kuna upungufu wa vyandarua,ndiyo nimeamua kuleta vyandarua ili watoto hawa wasije kupata ugonjwa wa malaria kwa kukosa vyandarua",alieleza Staadegaard.
“Taasisi hii yenye makao makuu yake nchini Uholanzi imeanzishwa mwezi Januari mwaka 2017 baada ya mimi kukutana na bwana Josephat Torner mkoani Geita kisha kujadili namna ya kushughulikia masuala mbalimbali yanayohusu watu wenye ualbino”,aliongeza Staadegaard.
Katika hatua nyingine alisema taasisi hiyo ina mpango kwa kuanza kununua Kahawa inayozalishwa nchini Tanzania na kuipeleka nje ya nchi kwa lengo la kuwainua kiuchumi watu wenye ualbino.
Naye Afisa Habari na Uhusiano kutoka Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania (TAS),Josephat Torner alisema katika kuadhimisha siku ya Albino duniani June 13 mwaka huu,TAS inaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya ualbino.
Kwa Upande wake Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Buhangija na msimamizi wa kituo hicho,Seleman Kipanya alishukuru kupokea msaada huo na kuwaomba wadau kuendelea kujitokeza kusaidia watoto hao.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE),Pieter Staadegaard akizungumza katika kituo cha kulelea watoto wenye ualbino cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga
Watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija
Afisa Habari na Uhusiano kutoka Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania (TAS),Josephat Torner akizungumza katika kituo cha Buhangija
Afisa Habari na Uhusiano kutoka Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania (TAS),Josephat Torner akizungumza kabla ya kuanza kugawa vyandarua
Vyandarua vilivyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE)
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE),Pieter Staadegaard akigawa vyandarua kwa watoto
Afisa Habari na Uhusiano kutoka Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania (TAS),Josephat Torner akiwaelekeza watoto wakati wa kugawa vyandarua
Zoezi la kugawa vyandarua linaendelea
Afisa Habari na Uhusiano kutoka Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania (TAS),Josephat Torner akigawa vyandarua
Msimamizi wa kituo cha Buhangija/Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Buhangija Seleman Kipanya akitoa shukrani baada ya kupokea msaada wa vyandarua
Mjumbe wa kamati ya shule ya msingi Buhangija Kuluthum Ally akitoa shukrani kwa taasisi ya JTFE kutoa misaada katika kituo cha Buhangija.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog