Mkurugenzi Mkuu wa Lake Fm Mwanza, Doreen Noni, akiwasilisha shukurani na salamu zake kwa niaba ya wafanyakazi wake kwenye burudani ya Gulio la Mtaa katika mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza.
#BMGHabari
102.5 Lake FM Mwanza, #RahaYaRockCity #RedioYaWananzengo jana Mei 26,2017 ilizindua rasmi burudani za Gulio la Mtaa kupitia kampeni yake ya usafi ya Ng'arisha Nzengo Uchafu Nuksi.
Burudani ilikuwa katika mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza kisha itahamia kwenye minada yote Jijini Mwanza ambapo kulikuwa na makumi ya wasanii walioshusha burudani kali balaa.
Kupitia burudani, Lake Fm inahamasisha suala la usafi minadani na mkoani Mwanza kwa ujumla. Pia kila mnada atakuwa akitafutwa Mama Lishe Bora, Balozi Imara na Mwananzengo Hodari na wote kujipatia zawadi nono.
Burudani za Gulio la Mtaa zimepewa nguvu na Pepsi, Tigo, Busy Bee, Barmedas Tv, Genic Studio, Mama Salakika Deco, Lake Zone Tents & Supply, Mamba Entertainment, CF Hospital, Gerusalem Sound na BMG.
Mkuu wa Vipindi, Lake Fm Mwanza, Yusuph Magupa akiwasilisha shukurani na salamu zake kwa niaba ya wafanyakazi wengine kwenye burudani ya Gulio la Mtaa katika mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza
Mkurugenzi wa Lake Fm, Doreen Noni (kushoto) akimpongeza Mama Lishe Bora, Neema Gerald, kutoka mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza na kumkabidhi zawadi yake
Mama Lishe kutoka mnada wa Nyakato National walipata zawadi kutoka Lake Fm
Wananzengo wakiburudika na show kutoka kwa mwanamuziki Abuu Mkali
Mwanamuziki Abuu Mkali kutoka Jijini Mwanza akiwaburudisha Wananzengo kwenye Gulio la Mtaa katika mnada wa Nyakato National.