Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu amefariki dunia leo saa nne asubuhi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
Mdogo wa marehemu, Shaibu Mwambungu amesema kaka yake alifariki dunia leo asubuhi baada ya hali yake kubadilika ghafla akiwa hospitalini hapo.
Shaib amesema taratibu za mazishi zitatolewa baadaye ambapo kwa sasa anajiandaa kusafiri kutoka Songea kuja jijini Dar es salam kwa ajili ya mazishi.