Aliyekuwa Mwandishi wa baba wa taifa Mwalimu julias Nyerere Paul sozigwa afariki dunia, alipokuwa akipatiwa matibabu kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Mtoto wa Mzee Sozigwa, Mchungaji Moses Sozigwa alisema tatizo la kwanza lililokuwa likimsumbua baba yao ni kupoteza kumbukumbu. Baadaye ilikuja kubainika ana tatizo la moyo, madaktari walisema moyo wake umekuwa mkubwa. Paul Sozigwa ndiye Katibu wa kwanza wa Rais (IKULU-HABARI).
Mbali na kuwa katibu wa Ikulu, nyadhifa nyingine alizoshika ni Mkurugenzi wa kwanza wa Redio Tanzania(RTD), DO Wilaya ya Kisarawe katika serikali ya kikoloni na katibu Mkuu, Wizara ya Habari na Utangazaji.
Kutoka kushoto: Habib Halala, Paul Sozigwa, Mwalimu J.K. Nyerere, Brig. Hashim Mbita na Benjamin Mkapa mwaka 1985.
Vilevile alishawahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya CCM zikiwemo za Mjumbe wa NEC, CC na M/kiti Tume ya Taifa ya Udhibiti na Nidhamu na M/kiti wa CCM mkoa wa Pwani.